Tuesday, March 08, 2016

KIVUKO CHA MV DAR ES SALAAM KUANZA KAZI HIVI KARIBUNI

Rais Dk. John Pombe  Magufuli akikagua kivuko cha MV Dar es salaam. 
…………………………………………………………………………………………………………………………
Na Raymond Mushumbusi MAELEZO
Kivuko cha Mv Dar es Salaam maarufu kama kivuko cha Rais Magufuli kipo katika matengenezo ya kawaida na kinatarajiwa kuanza kutoa huduma kama kawaida siku za hivi karibuni.
Akitoa ufafanuzi juu ya madai ya kutelekezwa kwa kivuko cha Mv Dar es Salaam katika maegesho yaliyopo kigamboni Jijini Dar es Salaam ,Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Manase Le-Kujan amesema sio kweli kwamba kivuko hicho cha Mv Dar es Salaam kimetelekezwa bali kimepumzishwa kutokana na matengenezo yaliyohitajika kufanywa katika kivuko hicho ili kuongeza ufanisi katika kutoa huduma kwa wasafiri.
“Sio kweli kwamba Kivuko cha Mv Dar es Salaam kimetelekezwa katika maegesho ya Kigamboni bali kimepumzishwa kwa muda kwa ajili ya matengenezo yake ya kawaida, hii ikiwa ni juhud
i ya kukiwezesha Kivuko hiki kuwa katika ubora unaotakiwa katika kutoa hudumazake”
“Mbali na matengenezo pia kuwepo kwa upepo mkali katika kipindi hiki cha mvua zinazoendelea imetufanya tukipumzishe kwa muda kivuko hicho” Alisema Mhandisi Manase.
Akifafanua zaidi,Mhandisi Manase amesema kuwa wapo katika mchakato wa kukipeleka kivuko hicho kwa ajili ya matengenezo makubwa Mjini Mombasa ili kukiongezea mwendo kasi na uhimili wake ili kiweze kuendana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia katika usafirishaji kwa kutumia vivuko na kuhuimili mabadiliko ya hali ya hewa.
Aidha amesema hakuna mvutano wa watendaji wakuu TEMESA wala madai yoyote ya kukisimamisha kwa makusudi kivuko hicho bali ni mpango wa TEMESA katika kukiboresha ili kiweze kuhudumia wananch iipasavyo.
Kivuko cha Mv Dar es Salaam hufanya safari zake za kusafirisha abiria kutoka Dar es Salaam kwenda Bagamoyo ikiwa ni juhudi za serikali za kupunguza tatizo la usafiri wa majini na kwa sasa kimesimama kwa muda kwa ajili ya matengenezoambayo yakikamilika kitaendelea kutoa huduma kama kawaida.
Ufanisi wa kivuko hiki utapunguza adha ya usafiri kwa wakazi wa Bagamoyo, Mbweni, Ununio, Boko, Bunju, Kunduchi na  Msasani wanaofanya safari zao kwenda Posta nakurudi sehemu wanakotokea. Na pia kitapunguza msongamano wa magari katika Barabara ya Ali Hassan Mwinyi kwani baadhi ya watu wataacha kutumia magari yao binafsi na kupanda kivuko hicho.
Post a Comment