Thursday, March 03, 2016

SERIKALI YAVIPONGEZA VYOMBO VYA HABARI KWA KUHABARISHA JAMII VYEMA.

bar1
Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Anastazia Wambura akisalimiana na Mkurugenzi mkuu National Media Group  Bw.Joe Muganda wakati wa tafrija fupi iliyoandaliwa na kampuni ya Mwananchi Communications limited kwa ajili ya Bodi ya  Mwananchi,wateja wake na wadau wa Habari.
bar2
Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Anastazia Wambura akiwasili katika hoteli ya Serena kwa ajili ya tafrija fupi iliyoandaliwa na kampuni ya Mwananchi Communications limited kwa ajili ya Bodi ya  Mwananchi,wateja wake na wadau wa Habari.
bar3
Mkurugenzi Idara ya Habari Maelezo Bw.Assah Mwambene (kushoto) akifurahia jambo na Mhariri Mtendaji wa Magazeti ya Mwananchi Communications Limited Bakari Machumu wakati wa tafrija fupi iliyoandaliwa na kampuni ya hiyo kwa ajili ya Bodi ya  Mwananchi,wateja wake na wadau wa Habari.
bar4
Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Anastazia Wambura akizungumza na wadau wa Habari wakati wa hafla fupi iliyoandaliwa na kampuni ya Mwananchi Communications Limited.Mheshimiwa wambura alivishukuru vyombo vya habari kwa kuhabarisha watanzania kipindi cha uchaguzi na pia katika siku mia za kwanza za Rais wa awamu ya tano na Mhe.John Pombe Magufuli na kuwapongeza kwa kuonyesha weledi na ukomavu katika uandishi wa Habari.
bar5
Wadau wa Habari wakifatilia hotuba ya Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Anastazia Wambura.Kutoka kushoto ni Bi.Teddy Mapunda na Mwisho kulia ni Maria Sarungi
bar6
Afisa Mtendaji mkuu wa Star Times Tanzania Bw.Leo Liofang(wa kwanza Kulia) pamoja na makamu wa Rais wa kampuni ya Star Times Bi. Zuhura Hanif(wa pili Kulia) wakifatilia jambo wakati wa tafrija fupi iliyoandaliwa na kampuni ya Mwananchi Communications limited kwa ajili ya Bodi ya  Mwananchi,wateja wake na wadau wa Habari.
Picha na Daudi Manongi.
……………………………………………………………………………………………………………………………
Na Daudi Manongi-WHUSM
Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia James Wambura amevipongeza Vyombo vya Habari kwa kuwahabarisha watanzania vyema katika mchakato wote wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 na katika kipindi cha siku mia za kwanza za awamu ya tano ya utawala wa Mheshimiwa Dr. John Joseph Pombe Magufuli.
Naibu Waziri uyo ameyasema hayo alipokuwa akiongea na wadau wa Habari katika tafrija fupi iliyoandaliwa na kampuni ya Mwananchi Communications Limited.
“Hakika mmeonesha uwezo mkubwa, weledi na ukomavu mkubwa wa kisiasa na uzalendo kwa nchi yetu”.Alisema Bi.Wambura.
Mhe.Wambura pia alieleza kuwa Serikali ya awamu ya tano ina dhamira ya dhati kabisa ya kushirikiana na wadau wote vikiwemo Vyombo vya Habari, ambapo pia mchakato wa Sheria ya Huduma za Vyombo vya Habari ambao ulishasomwa kwa mara ya kwanza bungeni bado Serikali inaendelea kupokea maoni ya wadau mbalimbali juu ya namna bora ya kuboresha Muswada huo.
Naibu Waziri uyo alikazia umuhimu wa upashaji habari na kusema ni jambo muhimu sana katika nchi yetu na kwaiyo Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo iko tayari kufanya kazi na wadau wote.
“Kama Serikali hatuwezi kuwakwepa wadau na ndio maana hata utaratibu wetu wa kushughulikia makosa kwenye Vyombo vya Habari umebadilika. Tumekuwa ni walezi zaidi badala ya kuwa viranja. Tunashauriana zaidi kuliko kutoa adhabu. Tunaelimisha zaidi kuliko kusubiliana”
Naibu Waziri uyo pia aliupongeza uongozi mpya wa jukwaa la wahariri na kuhaidi kuwapa ushirikiano wa karibu katika kutatua masuala mbalimbali ya Habari.
Kwa upande wake Mwenyekiti Mtendaji wa Bodi ya Magazeti ya Mwananchi Bw.Francis Nanai aliipongeza serikali kwa kuweka jitihada zaidi katika kuboresha mahusiano mazuri na vyombo vya Habari na pia kwa afrika mashariki Tanzania iko katika nafasi nzuri ukilinganisha na wenzetu katika suala la uhuru wa vyombo vya habari.

No comments: