Monday, March 21, 2016

RAIS DKT. JOHN POMBE MAGUFULI ATEKELEZA AGIZO LA MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM PAUL MAKONDA LA KUHAKIKI SILAHA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia kwa makini zoezi la uhakiki wa silaha zake lililokuwa likifanywa na Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Neema Laizer Ikulu jijini Dar es salaam. Mhe. Rais amekuwa mtu wa kwanza kutekeleza agizo la Mkuu wa Mko wa Dar es Salaam Paul Makonda.
Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Neema Laizer (kulia) akiendelea na zoezi la kuhakiki Silaha za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiitoa silaha yake aina Bastola kwa ajili ya uhakiki Ikulu jijini Dar es Salaam.
Kamanda wa Kanda Maalum ya Mkoa wa Dar es Salaam Kamishna CP Simon Sirro kulia akimkabidhi Silaha aina ya Bastola Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya uhakiki uliofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
Kamanda wa Kanda Maalum ya Mkoa wa Dar es Salaam Kamishna CP Simon Sirro kulia akimkabidhi silaha aina ya shortgun Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya uhakiki uliofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiiweka silaha yake vizuri mara baada ya kuhakikiwa Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiweka vizuri silaha yake aina ya Shortgun mara baada ya uhakiki uliofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza mara baada ya kumaliza zoezi la kuhakiki silaha zake Ikulu jijini Dar es Salaam. Mheshimiwa Rais amewataka wananchi wote wanaomiliki silaha kujitokeza kuhakiki silaha zao kama alivyoagiza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiweka vizuri silaha yake mezani kwa ajili ya uhakiki.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiweka dole gumba katika moja ya fomu za uhakiki Ikulu jijini Dar es Salaam. Picha na IKULU

No comments: