Saturday, March 12, 2016

WAZIRI WA MAJI AIAGIZA BODI YA DAWASCO KUWASIMAMISHA KAZI WATUMISHI WAKE KWA TUHUMA MBALIMBALI

Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Inj. Gerson Lwenge (katikati) akiongozana na Mwenyekiti wa bodi ya Shirika la Maji taka na Maji safi Dar es Salaam (DAWASCO) , Meja General (mstaafu), Samuel Kitundu (kushoto) na Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasco, Cyprian Luhemeja , wakati Waziri huyo alipoitembelea Dawasco leo na na kisha kutangaza watumishi tisa ambao ameiagiza bodi kuwasimamisha kazi kupisha uchunguzi dhidi yao kufuatia tuhuma mbalimbali. Mhandisi Lwenge alitembelea leo. 

WATUMISHI AMBAO WAZIRI AMEAGIZA BODI IWASIMAMISHE KAZI NI:-
Meneja Rasilimali Watu, Mvano Mandawa, Meneja Ufuatiliaji na Tathmini, Reinary Kapera, Teresia Mlengu, Emmanuel Guluba, Peter Chacha, Fred Mapunda, Reginald Kessy, Jumanne Ngelela na Bernard Nkenda. 

Aidha Waziri Lwenge aliagiza pia kuchunguzwa kwa CEO wa zamani Jackson Midala.

Miongoni mwa tuhuma zao ni pamoja na kufanya maunganisho ya maji yasiyofuata utaratibu kwa kampuni ya STRABAG inayotekeleza mradi wa mabasi yaendayo kasi na kusababisha kulikosesha shirika mapato yenye thamani ya sh Bilioni 2.8 (2,887,577,134/=). 
Mameneja wa Dawasco wakiwa katika mkutano huo.Baadhi yao walisimamisha kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazo wakabili.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Inj. Gerson Lwenge (kulia) akizungumza na bodi pamoja na menejimenti ya Shirika la Maji taka na Maji safi Dar es Salaam (DAWASCO) wakati Waziri huyo alipotembelea makao makuu ya shirika hilo Dar es Salaam jana na kuiagiza bodi kusimamisha kazi watumishi tisa. 
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Inj. Gerson Lwenge (aliyesimama) akizungumza na bodi pamoja na menejimenti ya Shirika la Maji taka na Maji safi Dar es Salaam (DAWASCO) wakati Waziri huyo alipotembelea makao makuu ya shirika hilo Dar es Salaam jana na kuiagiza bodi kusimamisha kazi watumishi tisa. 

No comments: