Thursday, March 10, 2016

DKT. POSSI AZINDUA KITABU CHA JINSI YA KUONDOKANA NA UMASIKINI

POS2
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Uratibu,Bunge,Kazi,Ajira na Walemavu Mhe. Dkt Abdallah Possi (Katikati) akikata utepe wakati wa uzinduzi wa kitabu kinachoelezea namna ya Tanzania inavyoweza kujiondoa katika umasikini na kuelekea kwenye ustawi uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
POS3
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Uratibu,Bunge,Kazi,Ajira na Walemavu Mhe. Dkt Abdallah Possi (wa pili Kushoto) akionesha kitabu kinachoelezea namna ya Tanzania inavyoweza kujiondoa katika umasikini na kuelekea kwenye ustawi katika uzinduzi uliofanyika leo Jijini Dare s Salaam Kushoto ni Mkuu wa Idara ya Uchumi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dkt Jehovanes Aikaeli wa pili kulia ni Prof Lician Msambichaka Mhariri Mkuu wa kitabu hicho na kulia ni Prof Delphin Rwegasira kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
POS4
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Uratibu,Bunge,Kazi,Ajira na Walemavu Mhe. Dkt Abdallah Possi ( wa pili kulia) akionesha kitabu pamoja na Mhariri Mkuu wa kitabu hicho nkwa washiriki na waandishi wa habari Prof Lician Msambichaka katika uzinduzi wa kitabu kinachoelezea namna ya Tanzania inavyoweza kujiondoa katika umasikini na kuelekea kwenye ustawi wa pili kushoto ni Mkuu wa Idara ya Uchumi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dkt Jehovanes Aikaeli na kushoto ni Mkuu wa Shule ya Sayansi na Jamii(UDSM) Prof Godius Kahyarara.
POS5
Baadhi ya washiriki toka Idara ya Uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wakimsikiliza Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Uratibu,Bunge,Kazi,Ajira na Walemavu Mhe. Dkt Abdallah Possi (Hayupo Pichani) wakati  kuzindua kitabu  kinachoelezea namna ya Tanzania inavyoweza kujiondoa katika umasikini na kuelekea kwenye ustawi uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
POS6
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Uratibu,Bunge,Kazi,Ajira na Walemavu Mhe. Dkt Abdallah Possi akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa uchumi kutoka Idara ya Uchumi Chuo Kikuu cha Dar es salaam mara baada ya kuzindua kitabu  kinachoelezea namna ya Tanzania inavyoweza kujiondoa katika umasikini na kuelekea kwenye ustawi uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Picha na Raymond Mushumbusi MAELEZO
………………………………………………………………………………………………………………….
Na Raymond Mushumbusi ,MAELEZO
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Uratibu,Bunge,Kazi,Ajira na Walemavu Mhe. Dkt Abdallah Possi amezindua kitabu kinachoelezea namna ya Tanzania inavyoweza kujiondoa katika umasikini na kuwa nchi ya uchumi wa kati.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Dkt Abdallah Possi amesema amefurahishwa sana kuona wasomi wa Tanzania wakijitolea muda wao na nguvu zao kushirikiana na Serikali katika kuondokana na umasikini ili tuelekee katika ustawi wa taifa.
“ Kitabu hiki kimekuja wakati muafaka ambapo Serikali ya awamu ya tano imejikita katika mapinduzi na maendeleo katika sekta ya viwanda ambayo imekuwa na mchango mkubwa katika maendeleo ya nchi nyingi duniani kwa sasa, hivyo tunaahidi kushirikiana na watafiti mbalimbali katika kutoa ufumbuzi wa changamoto zinazotukabili katika kuondokana na umasikini,”Alisema Dkt. Possi.
“ Nimekisoma hiki kitabu kwa ufupi na kuonda ni jinsi gani kitaweza kutusaidia katika mapambano dhidi ya umasikini lakini napenda kuwapa changamoto kuwa kazi hii ya kupambana na umasikini isiwe katika vitabu tu na sera bali iwe katika utekelezaji” Aliongeza Dkt Possi.
Naibu Waziri huyo ameongeza kuwa watafiti wa mambo ya uchumi wanatakiwa kuwashirikisha pia watu wenye ulemavu katika harakati za kuondokana na umasikini kwa kuwashirikisha katika uundwaji wa sera na utekelezaji wake katika kuleta maendeleo ya taifa.
Aidha Mhariri mkuu wa kitabu hicho, Prof Lucian Msambichaka amesema dhima kubwa ya kitabu hicho ni utekelzaji wa Sera,Mipango, Sheria na majukumu mbalimbali yahusuyo maendeleo kwa taifa na kuongeza kuwa kitabu hicho pia kimetoa njia bora na muafaka wa kukuza sekta ya viwanda, kuboresha huduma za jamii, kupunguza tatizo la ajira kwa vijana na jinsi gani Tanzania inavyoweza kunufaika na maliasilia zake katika kujileta maendeleo.
Kitabu hiki kimeandaliwa na Idara ya Uchumi ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kudhaminiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu. Kimeshirikisha waandishi zaidi ya 20 na kina kurasa zaidi ya 400 ambazo zimeelezea kwa kina namna ya kujikwamua kiuchumi kwa kuondokana na umasikini na kuelekea katika ustawi.

No comments: