Aliyekuwa Mgombea wa nafasi ya Meya wa Jiji la Dar es Salaam kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Mhe. Yenga Yusuph alipokuwa akiomba kura kwa wajumbe walioshiriki zoezi la kupiga kura ya kumchagua Meya leo jijini Dar es salaam.
Baadhi ya wabunge wa Chama cha Mapinduzi (CCM) walioshiriki zoezi la kupiga kura ya kumchagua Meya wa Jiji leo Dar es Salaam (Kushoto) ni Mbunge wa Jimbo la Ilala Mhe. Iddy Azzan Zungu na kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Segerea Mhe. Bonnah Kaluwa.
Baadhi ya wapiga kura waliohudhuria uchaguzi wa Meya wa Jiji la Dar es Salaam Leo 22/03/2016 wakifuatilia uchaguzi huo.
Baadhi ya Maafisa kutoka Ofisi za Jiji Dar es Salaam wakifuatilia Uchaguzi wa Meya uliyofanyika leo (kwa kwanza kulia) ni Afisa Sheria Mkuu Jumanne Mtinangi.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kikanda Mhe. Agustine Mahiga akizungumza na aliyekuwa Mgombea wa nafasi ya Meya wa Jiji kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Bw. Yenga Yusuph.
Mbunge wa Viti Maalum Kinondoni kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mhe. Suzan Lyimo (kushoto) pamoja na Mbunge wa jimbo la Kawe Mhe. Halima Mdee (CHADEMA) wakifuatilia zoezi la Upigaji kura wa kumchagua wa Meya leo jijini Dar es Salaam.
Mjumbe wa Kamati Kuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Edward Lowasa akimpongeza mshindi wa nafasi ya Umeya wa Jiji la Dar es Salaam Mhe. Isaya Chacha mara baada ya kutangazwa mshindi leo jijini Dar es Salaam.
Na Anitha Jonas – MAELEZO
………………………………………………….
Kaimu Mkurugenzi Jiji la Dar es Salaam Bi. Sara Yohana amemtanganza Mhe. Isaya Chacha Diwani wa Kata ya Vijibweni (CHADEMA) kutoka Manispaa ya Temeke kuwa Meya Mpya wa Jiji hilo.
Kaimu Mkurugenzi huyo alimtangaza Isaya kuwa mshindi mara baada ya uchaguzi huo kufanyika leo jijini Dar es Salaam ambapo mshindi alipata kwa kura 84 dhidi ya mgombea kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bw.Yenga Yusuph ambaye alipata kura 67 wakati kura 7 ziliharibika katika uchaguzi huo.
“Tunawashuruku wapiga kura wote mlioshiriki zoezi hili la upigaji kura kwa utulivu bila vurugu na kuweza kufanikisha mpaka kumpata Meya wa Jiji hili” alisema Bi Yohana.
Kwa upande wa mshindi wa Kiti cha Meya wa Jiji Mhe. Chacha aliwashukuru wapiga kura wake wa kata ya Vijibweni kwa kumchagua kuwa Diwani pamoja uongozi wa chama chake kukubali kumpa nafasi ya kugombea kiti hicho.
“Nimejipanga kuleta maendeleo katika sekta ya elimu pamoja na kupambana na kero ya foleni katika jiji letu na nitahakikisha wananchi wote maskini wanafaidika na mapato ya jiji hili ikiwemo kuendeleza miundombinu mbalimbali ,”alisema Chacha.
Aidha, Mwenyekiti wa CHADEMA taifa Bw.Freeman Mbowe alisema idadi ya wapiga kura tu inaonyesha wazi kuwa ushindi wa kiti hicho cha Meya ni lazima uchukuliwe na CHADEMA sababu madiwani wengi wa Mkoa wa Dar es Salaam wanatoka katika chama hicho.
Comments