Thursday, March 24, 2016

TUME YA UCHAGUZI YAKAMILISHA IDADI YA WABUNGE WA VITI MAALUMU WA TATU

Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi ya Taifa, Jaji Damiani Lubuva akizungumza na waandishi wa habari na kutangaza Majina ya wabunge wa wa viti maalumu katika ukumbi wa tume ya uchaguzi jijini Dar es Salaam, kuhusiana na tume hiyo kukamilisha idadi ya wabunge watatu wa viti maalumu wa Chama cha Mapinduzi(CCM) wawili na wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo chadema (Chadema) mmoja. Kushoto ni Mkuu wa Idara ya Habari na Elimu ya Mpiga Kura wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Givenes Aswile akiwa katika mkutano na waandishi wa habari leo.
Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi ya Taifa, Jaji Damiani Lubuva akitangaza majina ya wabunge wa viti maalumu watatu kuwa ni  Ritha Kabati (CCM), Oliver Semunguruka (CCM) pamoja na Lucy Owenya (Chadema). kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Kisheria wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Emmanuel Kavishe.
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi ya Taifa, Jaji Damiani Lubuva jijini Dar es Salaam leo wakati akitangaza majina ya wabunge wa viti maalumu
Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.


Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.
IDADI ya wabunge wa Viti Maalum watatu imekamilika baada ya uchaguzi majimbo yote  kufanyika ambapo Chama cha Mapinduzi (CCM) kimepata viti maalum viwili na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) mmoja.

Akizungumza leo na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Mstaafu ,Damian Lubuva amesema kuwa  uchaguzi umekamilika katika majimbo nane kwa kuwa na majimbo ya Tanzania Bara saba na Zanzibar Moja ambalo ni Jimbo la kijito Upele.

Viti vya wabunge wa viti maalum wanatokana na kura za jumla za wabunge wote na kuweza kupatikana viti hivyo.

Waliopatikana katika mchanganuo wa viti maalum ni, Ritha Kabati (CCM), Oliver Semunguruka (CCM) pamoja na Lucy Owenya (Chadema).

Lubuva amesema kuwa kufikia hapo ndipo uchaguzi umekamilika kutokana na viti hiyo kupatikana na kufanya kuwa viti maalumu 113 katika mgawanyo wa viti hivyo ni Chama cha Mapinduzi (CCM)  Viti  66,  cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)  viti 35 pamoja na Chama cha Wananchi (CUF)  viti 10.

Amesema kuwa kutokana na chaguzi zinazoendelea NEC ndiwe iwe sehemu ya usimamizi wa chaguzi zote.

Idadi kura za wabunge CCM katika uchaguzi ambazo zilibaki kutokana wagombea kufariki na kuarishwa kumeongeza viti maalum viwili.

No comments: