Friday, March 11, 2016

RAIS WA VIETNAM ATEMBELEA KAMPUNI YA SIMU YA HALOTEL JIJINI DAR ES SALAAM

Rais Truong Tang San akizindua Sanamu ya kiongozi wa zamani wa Vietnam iliyopo kwenye Kampuni ya Simu ya Halotel. 
Rais wa Vietnam, Mhe. Truong Tang San akizungumza na viongozi wa Kampuni ya Simu za mikononi kutoka nchini Vietnam ya Halotel inayofanya kazi hapa nchini Tanzania. Kampuni hiyo inatoa huduma ya simu Vijijini kwa gharama nafuu. Rais Truong Tang San anatarajiwa kumaliza ziara yake ya siku nne leo na kuelekea nchini Msumbiji kwa ajili ya ziara nchini humo. 
Viongozi mbalimbali walioambatana na Rais Truong Tang San, wakiwa pamoja na Balozi wa Vietnam, Mhe. Vothanh Nam (katikati) wakisikiliza kwa makini mazungumzo aliyokuwa yakiendelea kati ya Rais Tang San (hayupo pichani) na viongozi wa Kampuni ya simu ya Halotel 
Viongozi wa Halotel na Viongozi walioambatana na Rais Tang San (hayupo pichani) wakishangilia wakati uzinduzi ukiendelea 
Rais Truong Tang San akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Kampuni ya simu ya Halotel. 
Picha na Reginald Philip 

No comments:

RAIS DKT. SAMIA AKUTANA NA UJUMBE WA JUKWAA LA MABUNGE LA NCHI ZA MAZIWA MAKUU (FP-ICGLR) IKULU NDOGO TUNGUU, ZANZIBAR

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Kiongozi wa Jukwaa la Mabunge la...