Friday, March 04, 2016

UMOJA WA WANAWAKE TANZANIA (UWT) YAKABIDHIWA GARI MBILI ZENYE THAMANI YA SH MILIONI 22 NA MBUNGE WA VITI MAALUMU FAHARIA SHOMARI KHAMIS.

 Mbunge wa viti maalum, Faharia Khamis Shomari  akizungumza na Wajumbe wa Umoja wa WanawakeTanzania (UWT) katika ukumbi wa CCM Mkoa pichani hawapo kwenye sherehe ya makabiziano ya magari hayo yalio fanyika katika Ukumbi wa CCM Mkoa Amani Zanzibar.
 Mhe: Faharia  Shomari Khamis akimkabidhi funguo Mgeni Rasmi katika sherehe za Makabidhiano Naibu Katibu Mkuu CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai kwaajili ya kuwakabidhi wahusika.
 Naibu Katibu Mkuu CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai akitoa shukurani  kwa Mhe Faharia  na kuwataka wanawake wengine kuiga mfano wake wa kujitolea ndani ya chama,hafla ya Makabidhiano hayo ilifanyika katika ukumbi wa  CCM Mkoa Amani Zanzibar.
 Naibu Katibu Mkuu CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai akimkabidhi funguo za Gari Mwakilishi wa Umoja wa Wanawake UWT Tanzania Asha Mzee ambazo zimetolewa na Mhe. Faharia Shomari Khamis.

 Mwakilishi kutoka Umoja wa Wanawake UWT Tanzania, Asha Mzee akilifungua gari walilokabidhiwa na Mhe. Faharia  Shomar Khamis.
Magari aina ya Noha waliokabidhiwa Umoja wa Wanawake UWT Tanzania.(PICHA NA ABDALLA OMAR – HABARI MAELEZO ZANZIBAR).
Post a Comment