Monday, October 05, 2015

SMILE COMMUNICATIONS YAPANUA HUDUMA MTANDAO WAKE WA INTANETI YA 4G LTE KUFIKIA MIJI SABA TANZANIA

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dr. Ally Simba akizungumza kwenye hafla maalumu iliyoandaliwa na kampuni ya Smile Communications Tanzania kutangaza upanuzi wa huduma ya mtandao wake wa intaneti ya 4G LTE katika mikoa ya Mbeya, Mwanza, Moshi, Dodoma na Morogoro ikilenga kuleta mapinduzi katika utoaji wa huduma ya internet yenye kasi katika maeneo mengi zaidi nchini
Meneja Mkazi wa Smile Communications Tanzania, Bw. Eric Behner akizungumza kwenye hafla maalumu iliyoandaliwa na kampuni hiyo kutangaza upanuzi wa huduma ya mtandao wake wa intaneti ya 4G LTE katika mikoa ya Mbeya, Mwanza, Moshi, Dodoma na Morogoro ikilenga kuleta mapinduzi katika utoaji wa huduma ya internet yenye kasi katika maeneo mengi zaidi nchini.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dr. Ally Simba (mwenye tai nyekundu) akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa kampuni ya Smile Communications Tanzania kwenye hafla maalumu iliyoandaliwa na kampuni hiyo kutangaza upanuzi wa huduma ya mtandao wake wa intaneti ya 4G LTE katika mikoa ya Mbeya, Mwanza, Moshi, Dodoma na Morogoro ikilenga kuleta mapinduzi katika utoaji wa huduma ya internet yenye kasi katika maeneo mengi zaidi nchini.
Mkuu wa kitengo cha mauzo na masoko wa kampuni ya Smile Communications TanzaniaBw. Ahmed Seif , akizungumza kwenye hafla maalumu iliyoandaliwa na kampuni hiyo kutangaza upanuzi wa huduma ya mtandao wake wa intaneti ya 4G LTE katika mikoa ya Mbeya, Mwanza, Moshi, Dodoma na Morogoro ikilenga kuleta mapinduzi katika utoaji wa huduma ya internet yenye kasi katika maeneo mengi zaidi nchini.


KAMPUNI  ya Smile Communications Tanzania, imetangaza kupanua huduma ya mtandao wake wa intaneti ya 4G LTE katika mikoa ya Mbeya, Mwanza, Moshi, Dodoma na  Morogoro ikilenga kuleta mapinduzi katika utoaji wa huduma ya internet yenye kasi katika maeneo mengi zaidi nchini.

 Upanuzi huo ulitangazwa rasmi jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita kwenye hafla maalum iliyohudhuriwa na waandishi wa habari, wateja wa kampuni hiyo pamoja na wadau wa masuala ya teknolojia ya mawasiliano hapa nchini wakiongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dr. Ally Simba.

 Meneja Mkazi wa Smile Communications Tanzania, Bw. Eric Behner alisema fedha za uwezeshaji wa mradi huo ni sehemu ya Dola za Kimarekani milioni 365 ambazo kampuni mama ya Smile Telecoms ilikusanya mwezi Septemba kwa njia ya ukopaji na uuzaji wa hisa ili kufadhili upanuzi wa Intaneti yake ya kasi ya 4G LTE katika nchi za Afrika.

 “Hatua hii ni pamoja na upelekaji wa huduma zetu katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na zaidi inatizamiwa kuwa kufikia mwishoni mwa mwaka 2016, Smile Communications tutakuwa katika nafasi ya kutoa huduma za sauti na huduma za uhakika zitakazoweza kuwafikia watumiaji katika kila mkoa kati ya mikoa mitano iliyoainishwa nchini,’’ alibainisha.

 Uwekezaji huo unaelezwa kuwa ni moja kati ya ukuzaji mtaji mkubwa zaidi kuwahi kushuhudiwa na kampuni za mawasiliano barani Afrika na inapelekea jumla ya uwekezaji ulioelekezwa katika kutekeleza miradi ya Smile tangu kuanzishwa kwake mwaka 2007 na kufikia takribani Dola za Kimarekani milioni 600.

 Katika hatua nyingine kampuni hiyo ilitangaza huduma ya kipekee maalum kwa ajili ya wateja wa kibiashara iitwayo ‘Smile@business’ ambayo pamoja na mambo mengine, itatoa fursa kwa makampuni kulipia kifurushi kimoja kitakachotumika na watumiaji wengi bila kujali mahali walipo au kifaa wanachokitumia.

 “Lengo letu kuu ni kuwa chaguo la kwanza la watanzania katika huduma za intaneti ya kasi, na kuwatengenezea wateja wetu nchini njia ya haraka, ya kuaminika na yenye ubora wa hali ya juu katika kutekeleza majukumu yao ili kuleta maendeleo ya taifa kwa ujumla,’’ alisema Bw. Ahmed Seif , Mkuu wa kitengo cha mauzo na masoko wa kampuni hiyo.

 Akizungumza kwenye hafla hiyo, Dr. Simba alisema upanuzi huo wa huduma za kampuni ya Smile Communications Tanzania unakwenda sambamba na mpango wa serikali wa kuhakikisha kwamba huduma ya mawasiliano ya internet yenye kasi zaidi inafika kila kona ya nchi ndani ya kipindi kifupi kijacho.

 “Lengo ni kuona kwamba unafika wakati mtu aliyepo mkoa wa Katavi anakuwa kwenye mazingira ya kupata huduma ya internet yenye ubora na kasi sawa na mtu aliyepo jijini Dar es Salaam…ndio maana TCRA tunawapongeza sana watu wa Smile kwa hatua hii waliyofikia,’’ alibainisha.

No comments: