Wednesday, October 21, 2015

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AZINDUA MKONGO WA TAIFA WA MAWASILIANO, KATIKA KITUO CHA KUTUNZIA KUMBUKUMBU CHA TAIFA (NATIONAL INTERNET DATA CENTRE) KIJITOMYAMA.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifunua kitambaa kuzindua Jengo jipya la Mradi wa Kituo cha Kutunzia kumbukumbu Taifa (National Internet Data Centre) Kijitonyama, wakati wa hafla hiyo ya uzinduzi iliyofanyika leo Kijitonyama, jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Makame Mbarawa.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib, akipata maelezo kuhusu utendaji kazi wa mitambo ya kutunzia kumbukumbu, kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Huduma na Bidhaa za Shirika la Simu Tanzania, TTCL, Issaya Ernest, wakati Dkt Bilal, alipotembelea kituo hicho cha kutunzia kumbukumbu cha Taifa (National Internet Data Centre) Kijitonyama, leo Okt 21, 2015.

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Makame Mbarawa, kwa pamoja wakifunua kitambaa kuashiria uzinduzi rasmi wa Kituo cha kutunzia kumbukumbu cha Taifa (National Internet Data Centre) Kijitonyama, leo Okt 21, 2015. 

No comments:

RAIS SAMlA AFANYA MAZUNGUMZO NA MJUMBE MAALUM WA RAIS TSHISEKEDI

  Dar es Salaam, 26 Machi 2025 – Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan , amekutana na kufanya mazungu...