MAALIM SEIF ALIVYOPIGA KURA YAKE LEO

maalim seif

Mgombea urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad akipiga kura yake leo kwenye Kituo cha Mtoni, Chumba Na. 13, Zanzibar.
maalim seif 2
Mgombea urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad akipakwa wino baada ya kupiga kura yake leo.
maalim seif 4
Maalim Seif Sharif Hamad akiinua juu mkono wake baada ya kupakwa wino kuonyesha tayari amepiga kura yake.
maalim seif 3
Maalim Seif akiongea na wanahabari (hawapo pichani) mara baada ya kupiga kura.
Mgombea urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama cha Wananchi (CUF) ambaye ni Katibu Mkuu wa CUF na Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, tayari amepiga kura yake kwenye Kituo cha Mtoni, Chumba Na. 13 huko Zanzibar. Mara baada ya kupiga kura yake, Maalim Seif amesema kura yake ni siri yake lakini ana matumaini ya ushindi wa asilimia 72. (Picha Deutsche Welle)

Comments