Msafara wa mgombea wa Urais Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kwa tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufuli ukishuka kwenye kivuko cha Kamanga wilayani Sengerema mkoani Mwanza wakati mgombea huyo alipowasili wilaya ya Sengerema kwa ajili ya mikutano yake ya kampeni katika jimbo la Buchosa na Geita Vijijini ambapo amewahutubia wananchi katika mikutano miwili mikubwa ambayo imefanyika katika miji ya Nyehunge wilayani Sengerema na Nkome mkoani Geita.
Watu wengi wenojitokeza kwenye mkutano hiyo ambapo Dk. John Pombe Magufuli aliomba kura za ndiyo kwa wananchi ili wamchague na kuwa rais wa Tanzania katika uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu nchini kote ukishirikisha vyama vingi vya siasa
Dk John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi hao ambao wengi wao ni wavuvi amewaomba kutofanya uvuvi haramu kwani unasababisha kuua samaki na mayai yake jambo ambalo linapunguza samaki ziwani na kuwafanya wakose biashara lakini pia watakosa kitoweo.
Ameongeza kwamba Sangara mmoja anataga mayai zaidi ya milioni moja au milioni moja na laki tano, ukiua sangara kumi kwa bomu ni sawa na kuua samaki milioni kumi au kumi na tano ambao wangezaliwa jambo ambalo ni hasara kubwa kwa maliasili zetu za Samaki.
“Ninawaomba kura Ndugu zangu lakini lazima niwe mkweli na msema kweli ni mpezi wa Mungu, wavuvi wachache wanaofanya uvuvi haramu watubu na kuacha kazi hiyo. Kwani serikali yangu itaongozwa kwa kufuata sheria na Busara ya hali ya juu ili kuwafanya watanzania hasa wa maisha ya kawaida waone faida ya maliasili zao”.PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE -NKOME-GEITA
Msafara wa mgombea wa Urais Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kwa tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufuli ukiongoza na jeshi la polisi ili kuhakikisha usalama.
Mgombea wa Urais Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kwa tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufuli akielekea nje ili kusalimiana na wananchi wa kivuko cha Kamanga waliojitokeza waliojitokeza kumlaki.
Mgombea wa Urais Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kwa tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufuli akisalimiana na wakazi wa Kamanga mara baada ya kuwasili akitokea jijini Mwanza
mgombea wa Urais Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kwa tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi na kuomba kura katika mji wa Nyehunge jimbo la Buchosa mkoani Mwanza.
Mgombea wa Urais Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kwa tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufuli akisisitiza jambo katika mkutano huo.
Umati wa wananchi wa Nyehunge Buchosa wakimshangilia mgombea wa Urais Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kwa tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufuli alipokuwa akiwahutubia katika mkutano wa kampeni.
Mgombea wa Urais Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kwa tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufuli akimnadi mgombea ubunge wa jimbo la Buchosa Mh. Charles Tizeba katika mkutano wa kampeni uliofanyika mjini Nyehunge.
Mgombea wa Urais Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kwa tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufuli akimnadi mgombea ubunge wa jimbo la Buchosa Mh. Charles Tizeba wakati alipomuombea kura katika mkutano wa kampeni uliofanyika Nyehunge.
Mgombea wa Urais Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kwa tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwa amekaa na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza na mjumbe wa kamati ya ushindi ya CCM Mh. Anthony Dialo kulia na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Geita na mgombea ubunge jimbo la Geita vijijini Ndugu Joseph Kasheku Msukuma katikati katika mkutano wa kampeni uliofanyika mji wa Nkome Geita vijijini.
Baadhi ya wananchi wenye ulemavu wakimshangilia Dk. John Pombe Magufuli wakati alipokuwa akihutubia mkutano wa kampeni mjini Nkome Geita vijijini.
Kundi la Makomando likitoa burudani katika mkutano huo.
Msanii Malaika akifanya vitu vyake katika mkutano huo.
Kundi la Orijino Kemedi likionyesha vitu vyao jukwaani.
Masanja Mkandamizaji na Mpoki wakihutubia wananchi kama kawaida yao.
Mgombea wa Urais Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kwa tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufuli akisisitiza jambo wakati alipokuwa akihutubia mkutano huo mjini Nkome.
Mbwembwe za kampeni kama unavyowaona katika picha.
Mgombea wa Urais Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kwa tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufuli kwa mbali akionekana wakati alipokuwa akihutubia maelfu ya wananchi mjini Nkome Geita Vijijini.
Picha mbalimbali zikionyesha maelfu ya wananchi waliohudhuria katika mkutano huo.
Comments