Saturday, October 17, 2015

DKT SHEIN AMNADI DKT MAGUFULI KISIWANI UNGUJA LEO,ASEMA ANATOSHA KUWA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

Mgombea
Urais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt Mohamed Shein akimnadi
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama cha
Mapinduzi CCM Dkt John Pombe Magufuli mbele ya maelfu ya wananchi
waliohudhuria mkutano wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya Mnazi
Mmoja,kisiwani Unguja jioni ya jana
.

Dkt
Shein emebainisha wazi kwenye mkutano huo wa kampeni kuwa Dkt Magufuli
ni mtu sahihi na anatosha kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania,amesema kuwa iwapo atachaguliwa kuwa Rais wa awamu ya tano
atashirikiana nae kwa kila jambo kuhakikisha Tanzania inapiga hatua
zaidi kimaendeleo.
Mgombea
Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama cha
Mapinduzi CCM Dkt John Pombe Magufuli akihutubia maelfu ya wananchi
waliohudhuria mkutano wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya Mnazi
Mmoja,kisiwani Unguja jioni ya jana.PICHA  ZOTE NA MICHUZI JR-KISIWANI UNGUJA.
Sehemu
ya umati wa wakazi wa Kisiwani Unguja na vitongoji vyake wakiwa
wamejitokeza kwa wingi katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika
viwanja vya Mnazi Mmoja mjini humo,ambapo Mgombea Urasi wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania kupitia chama cha CCM Dkt John Pombe Magufui
aliwahutubia.
Mgombea
Urais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt Mohamed Shein
akimsikiliza kwa makini Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi CCM Dkt John Pombe Magufuli kabla ya
kupanda jukwaani na kuwahutubia maelfu ya wakazi wa kisiwani Unguja
kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya Mnazi
Mmoja,kisiwani humo.
Wananchi wa kiswani Unguja wakishangilia jambo kwenye mkutano huo wa kampeni.
Mgombea
Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama cha
Mapinduzi CCM Dkt John Pombe Magufuli akihutubia maelfu ya wananchi
waliohudhuria mkutano wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya Mnazi
Mmoja,kisiwani Unguja jioni ya jana.
Rais
Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,Mh Al Hassan Mwinyi
akiwahutubia Wananchi (hawapo pichani) ,kwenye mkutano wa kampeni
uliofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja,kisiwani Unguja jioni ya jana.
Mwenyekiti
wa CCM Mkoa wa Mjini,Ndugu Boraafya Silima akizungumza machache kwenye
mkutano wa kampeni kabla ya kumkaribisha Mgombea Urais wa CCM Dkt
Magufuli kuwahutubia wananchi wa kisiwani Unguja.
Nyomi la wakazi wa Kisiwani Unguja ndani ya mkutano wa kampeni.
Sehemu ya umati wa wakazi wa kisiwani Unguja na vitongoji vyake wakiwa  wamekusanyika kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja,kisiwani Unguja jioni ya jana.
Baadhi ya Wafuasi wa chama hicho wakishangilia jambo kwenye mkutano wa kampeni wa Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli
Wadau wakifuatilia mkutano wa kampeni ndani ya uwanja wa Mnaji Mmoja kisiwani Unguja.
Rais
Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,Mh Al Hassan Mwinyi
akiwahutubia Wananchi (hawapo pichani) ,kwenye mkutano wa kampeni
uliofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja,kisiwani Unguja jioni ya jana.
 wakifuatilia mkutano wa kampeni.
Mgombea
Urais wa Jamhuri ya Muungano Dkt Jonh Pombe Magufuli akiwapungia
wananchi wa Kisiwani Unguja (hawapo pichani),alipokuwa akiwasili kwenye
mkutano wa kampeni katika viwanja vya Mnazi Mmoja mjini humo.
Balozi
Seif Ali Iddi akiwahutubia wananchi wa Kisiwani Unguja kwenye mkutano
wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya Mnazi mmoja.
Baadhi ya Wafuasi wa chama hicho wakifurahia jambo kwenye mkutano wa kampeni wa Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli
Sehemu ya umati wa wakazi wa kisiwani Unguja na vitongoji vyake wakiwa  wamekusanyika kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja,kisiwani Unguja jioni ya jana.
Wananchi wa Kisiwani Unguja wakifuatilia mkutano wa kampeni ndani ya viwanja vya Mnazi Mmoja.

No comments: