Monday, October 19, 2015

SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA LATOA CHANGAMOTO VIJANA WALIOACHA KUTUMIA MADAWA YA KULEVYA

Kwaya ya KKKT Keko, Dar es Salaam ikitumbuiza katika tamasha la vijana walioamua kuacha dawa za kulevya lililofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee lengo likiwa ni kuchangisha kiasi cha shilingi milioni 300 kwaajili ya kujenga kituo cha kuhudumia vijana hao walioathirika na dawa ya kulevya. Tamasha liliandaliwa na Kanisa la KKKT kupitia kitengo chake cha kuhudumia makundi maalumu likiwamo la vijana hao. Shirika la nyumba katika hafla hiyo lilichangia fedha, mashine nne zitakazoajiri vijana 40.
Meneja wa Huduma kwa Jamii wa Shirika la Nyumba la Taifa, Muungano Saguya ambaye pia aliyemwakilisha mgeni rasmi wa tamasha hilo Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Nehemia Kyando Mchechu akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, Paul Makonda ambaye alikuwa mgeni mashuhuri wa hafla hiyo pia ni mmojawapo wa wapambanaji dhidi ya madawa ya kulevya akizungumza na walioffika alitoa ahadi ya mifuko 100 kwaajili ya ujenzi wa kituo cha vijana hao walioacha dawa za kulevya kwa hiyari bila kutumia dawa nyingine.
 Meneja wa Huduma kwa Jamii wa Shirika la Nyumba la Taifa, Muungano Saguya ambaye pia aliyemwakilisha mgeni rasmi wa tamasha hilo Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Nehemia Kyando akiwa katika meza kuu, kulia kwake ni Yahya Charahani, Meneja Mawasiliano wa NHC.
 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda ambaye alikuwa mgeni mashuhuri wa hafla hiyo pia ni mmojawapo wa wapambanaji dhidi ya madawa ya kulevya akiimba wimbo katika jukwaa kutumbuiza waalikwa wa shughuli hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akiserebuka na vijana walioacha madawa ya kulevya na sasa kujishughulisha na shughulia mbalimbali za kujiongezea kipato.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, Paul Makonda ambaye alikuwa mgeni mashuhuri wa hafla hiyo akisalimiana na  Meneja wa Huduma kwa Jamii wa Shirika la Nyumba la Taifa, Muungano Saguya ambaye pia alikuwa Mgeni Rasmi kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa NHC.

Vijana walioacha madawa ya kulevya kutoka mkoani Morogoro na sasa kujishughulisha na shughulia mbalimbali za kujiongezea kipato wakiserebuka kwa kuimba nyimbo za injili kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jana..
 Vijana walioacha madawa ya kulevya kutoka mkoani Kigogo, Luhanga na sasa kujishughulisha na shughulia mbalimbali za kujiongezea kipato wakiserebuka kwa kuimba nyimbo za injili kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jana. wanaongozwa na mlezi wao ambaye ndiye mratibu mkuu wa tamasha hilo Mchungaji Kiongozi Usharika wa Kigogo, Richard Hananja.
 Vijana walioacha madawa ya kulevya kutoka Bagamoyo mkoani Pwani na sasa kujishughulisha na shughulia mbalimbali za kujiongezea kipato wakiimba wimbo wa injili kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jana.
Kiongozi wa vijana hao aliyeacha matumizi ya madawa ya kulevya akikabidhi risala kwa mgeni rasmi.
 Meneja wa Huduma kwa Jamii wa Shirika la Nyumba la Taifa, Muungano Saguya ambaye pia alikuwa Mgeni Rasmi kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa NHC akitoa hotuba kwa umati uliofika ukumbini hapo.
Umati wa watu waliofika katika ukumbi huo ukifuatilia matukio yaliyokuwa yakiendelea ukumbini hapo.

No comments: