Thursday, October 15, 2015

UWT KINONDONI WALIVYOMUENZI NYERERE

1MWENYEKITI WA Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), Wilaya ya Kinondoni, Frolance Masunga, akihutubia wanachama wa umoja huo, katika mkutano wa hadhara ulioandaliwa maalumu kwaajili ya kumbukumbu ya miaka 16 ya kifo cha Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Nyerere, karibu na nyumba ya makumbusho aliyokuwa akiishi Mwalimu iliyopo Kata ya Mzimuni, barabara ya Makumbusho, mtaa wa Ifunda, Magomeni, Dar es Salaam, juzi. Wengine walioka mbele ni Mstahiki Meya wa Kinondoni, Yusuf Mwenda, Kada wa CCM Hassan Dalali, Mgombea Udiwani kata ya Mzimuni (CCM) Chambuso Mohamed.
2KAIMU Mkurugenzi wa kituo cha Radio Uhuru FM, Angel Akilimali (kulia) akimkabidhi msaada wa cherehani yenye tahami ya Sh.300,000, Asha Yusuf mwenye ulemavu wa miguu mkazi wa Buguruni, ulitolewa na kituo hicho kupitia kipindi cha Wnawake na Maendeleo, Dar es Salaam, jana. Wengine ni wafanyakazi wa kituo hicho.
……………………………………………………………………
Na Mwandishi Wetu
UMOJA Wanawake Tanzania (UWT), Wilaya ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam, umeadhimisha miaka 16 ya kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa kufanya mkutano mkubwa wa hadhara katika kata ya Mzimuni, Magomeni karibu na nyumba aliyokuwa anaishi Mwalimu, iliyopo Mtaa wa Makumbusho, Barabara ya Ifunda namba 62. 
UWT pia walitembelea nyumba hiyo na kujionea mambo mbalimbali yanayogusa maisha halisi ya Mwalimu.
Katika hotuba yake, Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Kinondoni, Florance Masunga alisema kuwa njia pekee ya kumuenzi Mwalimu ni kudumisha, amani, upendo na mshikamano pamoja na kukipigia kura Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 25, mwaka huu.
Frolance, alisema, UWT inatambua mchango mkubwa alioutoa hayati Baba wa Taifa ikiwemo kuliachia taifa tunu muhimu ambazo ni amani, upendo na mshikamano ambavyo vinatakiwa kuendelezwa na watanzania wote ikiwa ni njia muhimu ya kumuenzi.
“Njia nyingine ya kumuenzi hayati Baba wa Taifa ni kuwachagua wagombea wa CCM katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 25, mwaka huu. Wanawake tujitokeze kwa wingi kumpigia kura Dk. John Maguful, wabunge na madiwani. Nyerere alipenda uadirifu na hizi ndiyo sifa alizonazo Dk. Magufuli. Ni mchapakazi, mpenda watu, hana makundi na anania ya kweli ya kutuletea mabadiliko. Shime wanawake na watanzania wote kwa ujumla Oktoba 25 kura zote ni kwa Dk. Magufuli,”alisema Florance.
Aidha, alisema kuwa uwepo wa UWT unatokana na hayati Baba wa Taifa kuthamini usawa katika uongozi, ambapo CCM ndiyo chama pekee ambacho kimekuwa kikienzi hatua hiyo ambapo kwa mwaka huu kimemsimamisha Samia Suluhu Hassan kuwa mgombea mwenza wa urais.
“Tukimchagua Dk. Magufuli kwa kura nyingi tutamwezesha ia Samia kuwa Makamu wa Rais. Atatusaidia kututatulia changamoto zetu. Wanawake tusipoteze nafasi hiyo muhimu. Oktoba 25 tuwashawishi waume zetu na wanafamilia kuichagua CCM kura zetu kwa Kinondoni ni kwa mgombea ubunge wetu Idd Azzan na madiwani wote wa CCM.
Mstahiki Meya wa Halmshauri ya Manispaa ya Kinondoni, Yusuf Mwenda, ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mkutano huo, alisisitiza kuwa, Baba wa Taifa alikuwa ni kielelezo cha umoja, amasni na utulivu hivyo kuitaka jamii kuendelea kumkumbuka.
“Mwalimu aliishi hapa Magomeni eneo la Mzimuni. Sifa kubwa aliyokuwa nayo ni uadirifu.Tunapoelekea katika uchaguzi mkuu Otoba 25 mwaka huu ni lazima tuchague viongozi waadirifu. Katika wagombea nane wa urais mgombea muadirifu ni Dk. Magufuli pekee. Watanzania tukichagua kwa kufuata uadirifu basi kura zetu zote ni kwa Dk. Magufuli. Hata kama kuna wapinzani CUF, CHADEMA,NCCR na vyama vingine msipoteze kura zenu kuwapigia wagombea ambao hawatashinda. Piga kura yako kwa rais ajaye Dk. Magufuli ili kura yako iwe na thamani,”alisema Meya Mwenda.
Alisema, Dk. Magufuli ataongoza nchi kwa haki na usawa bila kujari tofauti ya itikadi, dini, ukabila na ni mchapakazi.

No comments: