MAGUFULI ALIVYOLITIKISA JIJI LA MWANZA, AKINA MAMA WATANDIKA VITENGE VYAO ILI APITE, WENGINE WAPIGA STAILI YA “MAGUFULIKA”
Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa jiji la Mwanza waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika kwenye viwanja vya Furahisha.(ADAM MZEE NA JOHN BUKUKU -FULLSHANGWE-MWANZA)
Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufuliakihutubia wakazi wa jiji la Mwanza ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa anataka kuibadilisha Mwanza na kuwa jiji kubwa la kibiashara.
Uati uliojitokeza kwenye viwanja vya Furahisha kumsikiliza Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufuli.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Fid Q akiburudisha wakazi wa jiji la Mwanza waliojitokeza kumsikiliza Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufuli kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika viwanja vya Furahisha.
Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufuliakiwanadi wagombea ubunge wa jimbo la Ilemela na Nyamagana kwenye uwanja wa Furahisha.
Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufuli akimkabidhi kitabu cha Ilani ya Uchaguzi mgombea ubunge wa jimbo la Nyamagana kupitia CCM Ndugu Stanslaus Mabula.
Mgombea ubunge wa jimbo la Ilemela Mama Angelina Sylvester Lubala Mabula akihutubia wakazi wa jiji la Mwanza waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa kampeni za kumnadi mgombea Urais upitia CCM Dk. John Pombe Magufuli.
Mgombea ubunge wa jimbo la Nyamagana kupitia CCM Ndugu Stanslaus Mabula akihutubia umati wa wakazi wa jiji la Mwanza na kuahidi kuwatumikia wakazi wa jimbo lake kwa nguvu zake zote.
Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufuli akiondoka kwenye viwanja vya Furahisha mara baada ya kumaliza kuhutubia wakazi wa jiji la Mwanza.
Dk. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wananchi wakati msafara wake ulipokuwa ukielekea kwenye viwanja vya Furahisha kwa ajili ya mkutano wa kampeni jijini Mwanza Jana.
Bodaboda hawakutulia kabisa barabarani ili mradi walihakikisha wamemfikisha Tingatinga kwenye viwanja vya Furahisha.
Baadhi ya wananchi wakimshangilia Dk. John Pombe Magufuli wakati aliposimama eneo la Pansiansi ili kuwasalimia wananchi akitokea uwanja wa ndege wa Mwanza kuelekea Uwanja wa Furahisha Mwanza.
Akina mama wengine walikuja na ndoo za maji ili mradi wasafishe barabara ambayo alikuwa akipita Dk. John Pombe Magufuli.
Maafisa wa Usalama walikuwa makini kuhakikisha kila jambo linakwenda sawa.
Hapa Dk. John Pombe Magufuli akiingai uwanja wa Furahisha.
Bendera za rangi ya kijani na njano zilitawala mkutano wa Dk. John Pombe Magufuli..
Dk. John Pombe Magufuli akicheza kwa furaha wimbo wa TOT mara baada ya kuwasili kwenye jukwaa la mkutano huo uliojaa wananchi kupita kiasi.
Mwenyekiti wa CCM mkoani Mwanza na Mjumbe wa Kamati ya Ushindi ya CCM Ndugu Anthony Dialo akimkaribisha Dk. John Pombe Magufuli.
Mkuu wa Msafara na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM Alhaji Abdallah Bulembo akimpigia debe Dk. John Pombe Magufuli.
Chege na Temba wasanii wa muziki wa Kizazi kipya ktoka kundi la TMK Family wakisumbua jukwaani kwa burudani yao kali.
Tinga Tinga likiwa limeegeshwa kwenye uwanja wa Furahisha mjini Mwanza kama ishara ya kumkubali Dk .John Pombe Magufuli.
Akina mama wa Mwanza wakitandika vitenge na kanga ili mradi mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli anapita hii ilikuwa mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Mwanza leo.
Mama Akimagufulika ili kuonyesha hisia zake kwa CCM mara baada ya kuona msafara wa Dk. John Pombe Magufuli akitoka kwenye uwanja wa Ndege wa Mwanza.
Mkurugenzi wa Jembe FM Bw. Sebastian Ndege kulia akiwa na wasanii Richie One katikati na Juma Nature wa pili kutoka kushoto katika mkutano wa kampeni wa Dk. John Pombe Magufuli jijini Mwanza, kushoto ni mwana CCM Kindakindaki.
Comments