Saturday, October 31, 2015

TACCEO YALAANI KITENDO CHA POLISI KUVAMIA OFISI YAO NA KUWAKAMATA WAANGALIZI WA UCHAGUZI MKUU

Mmoja wa Wakurugenzi wa Mtandao wa Asasi za Kiraia za Uangalizi wa Chaguzi (TACCEO), Hebron Mwakagenda (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Makao Makuu ya Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu Dar es Salaam leo mchana, kuhusu Polisi kudaiwa kufanya uvamizi na kuwakamata waangalizi, vifaa binafsi na vifaa vya Kituo cha Uangalizi wa Uchaguzi Mkuu wa 2015 katika kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Mbezi jijini Dar es Salaam. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa LHRC, Imelda Urrio na Kaimu Mkurugenzi wa Utetezi wa LHRC, Anna Henga
Kaimu Mkurugenzi wa LHRC, Imelda Urrio (wa tatu kutoka kushoto), akisisitiza jambo katika mkutano huo. Kutoka kulia na Mwanasheria wa LHRC, Halord Sungusia, Mwakilishi wa Taasisi ya YPC, Maria Kayombo na Mwakiliashi wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP),Melikizedeck Karol.
Mkutano na waandishi wa habari ukiendelea.

TACCEO yalaani kukamatwa waangalizi wa uchaguzi

Na Dotto Mwaibale
ASASI za Kiraia za Uangalizi wa Uchaguzi (TACCEO), pamoja na Kituo cha Haki za Binadamu (LHRC), wamelaani kitendo cha kuvamiwa na Jeshi la Polisi, Oktoba 29, mwaka huu na lile la kukamata vitendea kazi na waangalizi wa uchaguzi  36.
Akizungumza jijini Dar es Salaam leo mchana, Kaimu Mwenyekiti wa TACCEO, Hebron Mwakagenda, alisema Jeshi la Polisi lilivamia kituo cha LHRC, kilichopo Mbezi na kudai kuwa, waliagizwa na mamlaka husika kuwakamata waangalizi  na vifaa vya kieletroniki vilivyokuwa vikitumika katika mchakato huo.
Mwakagenda alisema polisi hao waliongozwa na Mkuu wa Upelelezi Wilaya  ya kipolisi Kawe, ASP Mgonja, ambapo  maofisa wa uangalizi walieleza kuwa, walipata taarifa kituo hicho kinakusanya na kunasambaza taarifa za matokeo zisizo rasmi.
"Katika mchakato huo, polisi walikusanya vifaa vyetu na kukamata kompyuta za mezani 24, mpakato tatu na simu za mkononi za waangalizi 25," alisema Mwakagenda.
Alisema baada ya tukio hilo, vifaa hivyo vilichukuliwa na kukabidhiwa kituo cha kati na baadaye kupelekwa makao makuu ya jeshi la polisi huku, baadhi ya waangalizi wakichukuliwa kwa ajili ya kutoa maelezo na baadaye kupata dhamani.
Watu hao wametakiwa kurudi kituoni hapo Oktoba 30, mwaka huu kwa ajili ya kumalizia maelezo yao.
"Mchakato huo la kurudi Oktoba 30, mwaka huu lilifanikiwa na kwa sasa waliambiwa warudi leo, kwa taratibu nyingine za kipolisi," alisema Mwakagenda.
Mwakagenda alisema uvamizi huo uliofanywa na jeshi la polisi ni wa kudhoofisha ustawi wa demokrasia nchini kwani, wasababisha kuwatishia wananchi kushiriki katika mambo yanayohusu mchakato wa chaguzi nchini.
"Katika hili ni kama wameondoa dhana nzima ya ushiriki kikamilifu wa sekta ya umma na binafsi   katika kutoa maoni ya kuboresha demokrasia na uchaguzi," alisema Mwakagenda.
Aidha, Mwakagenda alisema uvamizi huo uliathiri  na kuwafanya wakashindwa kukusanya taarifa za mwisho za uangalizi wa matokeo na ukusanyaji wa maoni ya wananchi.
"Uangalizi kwa kutumia tehama haujaanza mwaka huu kwani, tangu mwaka 2010 kulikuwa na utaratibu huu, mambo yaliyofanyika hivi sasa tunashindwa kuelewa tatizo ni nini," alisema

No comments: