Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula (kulia ) akizungumza na Msaidizi wa Rais wa masuala ya Kidplomasia, Zuhura Bundara (kushoto). Katikati ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano cha wizara hiyo, Mindi Kasiga.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Philippines nchini Bayani Mangibin mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dares Salaam Oktoba 29, 2015 kwa ajili ya kukabidhi hati ya utambulisho kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Kikwete.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Misri nchini Yasser Ahmed Elshawaf mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dares Salaam Oktoba 28, 2015 kwa ajili ya kukabidhi hati ya utambulisho . Kulia wa pili ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amepokea hati za utambulisho kutoka kwa mabalozi wanne wanaziwakilisha nchi zao hapa Tanzania.Mabalozi waliowasilisha hati zao kwa Rais Kikwete ikulu Jijini Dar es Salaam Oktoba 28, 2015 ni pamoja Mhe.Yasser Ahmed Al Eldin Elshawaf Balozi mpya wa Misri hapa nchini, Mhe.Yahel Vilan Balozi mpya wa Israel nchini Tanzania, Mhe.Bayani Mangibin balozi mpya wa Ufilipino nchini na Mhe. Tan Puay Hiang Balozi mpya wa Singapore nchini Tanzania.
Comments