Wednesday, October 21, 2015

WADAU WA AMANI MKOA WA SHINYANGA WAKUTANA KUJADILI JINSI YA KUDUMISHA AMANI KIPINDI CHA UCHAGUZI

Hapa ni katika ukumbi wa Vigirmark Hotel mjini Shinyanga ambako jana Jumanne,Oktoba 20,2015,wadau mbalimbali wa amani mkoani Shinyanga wamekutana kwa ajili ya majadiliano ya ushirikiano wa kudumisha amani katika kipindi cha uchaguzi mkuu 2015. Kikao hicho kimeandaliwa na uongozi wa mkoa wa Shinyanga likiwemo jeshi la polisi kwa kushirikiana na Shirika la Save The Children linalojihusisha na utetezi wa haki za watoto.

Mambo kadha wa kadha yamejadiliwa ikiwemo kuhakikisha ulinzi na usalama wa watoto kabla,wakati na baada ya uchaguzi,lakini pia viongozi wa vyama vya siasa,wagombea na wanachama kuheshimu na kutekeleza sheria,kanuni,maadili na maelekezo ya tume ya taifa ya uchaguzi pamoja na sheria nyinginezo za nchi katika kipindi chote cha uchaguzi.
Mgeni rasmi katika kikao hicho alikuwa mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama mkoa. Fuatilia matukio katika picha hapa chini-Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blogMgeni rasmi ambaye ni mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga akifungua kikao hicho cha wadau ambapo pamoja na mambo mengine alisisitiza kuwa serikali haiko tayari kuona amani ya nchi inavurugwa hivyo itachukua hatua kali za kisheria kwa watu wote watakaofanya vurugu siku ya uchaguzi.Mgeni rasmi ambaye ni mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga akizungumza katika kikao hicho ambapo alisema ofisi yake imepata taarifa kuwa kuna baadhi ya wagombea wanatembea na silaha za moto,mapanga,manati na kufundisha vijana mbinu za kuvunja amani siku ya uchaguzi.Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga akisisitiza kuwa watu wote waliojiandikisha wana haki ya kupiga kura Oktoba 25,2015 na kuwataka baadhi ya watu wanaojipanga kukaa mita 200 kutoka kituo cha kupigia kura kuachana na wazo hilo na badala yake waendelee tu shughuli zao na wakati muda wa kutangazwa matokeo ndiyo warudi vituoniWadau wa mkutano huo walisisitiza umuhimu wa wananchi kupiga kura kisha kuendelea na shughuli zao Oktoba 25,2015 badala ya kukaa mita 200/300 kutoka kwenye kituo cha kupigia kura kwa vile kila chama kitakuwa na wakala wake hao ndiyo wataweza kulinda kura zao .Kushoto ni kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Justus KamugishaWadau wakiwa ukumbini,kulia ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro.Wadau wa amani mkoani Shinyanga pia walikubaliana kukabiliana na watu wote wanaopanga kuvuruga amani ya nchi wakati wa uchaguzi. 
Post a Comment