AJALI YA HELIKOPTA ILIYOPOTEZA MAISHA YA DEO FILIKUNJOMBE


Asakari polisi na wataalamu wakikagua mabaki ya chopa namba  5Y-DKK iliyoanguka juzi jioni ikitokea Dar kuelekea Ludewa sehemu ya hifadhi ya wanyama ya Selous ambapo Mbunge wa Ludewa Deo Filikunjombe, rubani Capt. William Slaa na abiria wengine wawili - Casablanca Haule na Ngondombwitu Nkwera - walipoteza maisha.
 Timu ya waokoaji wakibeba mabaki ya miili ya marehemu
 Askari wakiwa eneo la ajali 





Mbunge wa Ludewa Mhe Deogratias Haule Filikunjombe (chini) amefariki dunia katia ajali ya Chopa katika hifadhi ya wanyama ya Selous, pamoja na rubani Kepteni William Silaa (juu kulia), mfanyakazi wa halmashauri ya wilaya ya Ludewa na ndugu yake Marehemu Filikunjombe ambao majina  hayajapatikana mara moja.

Mhe. Deo Filikunjombe, rubani na  na abiria wengine walipata matatizo ya engine ya chopa namba  5Y-DKK juzi jioni wakitokea Dar kuelekea Ludewa.

Kwa mujibu wa Meya wa Ilala aliyemaliza muda wake Mhe Jerry Silaa, ambaye ni mtoto wa rubani, hakuna mtu aliyenusurika katika ajali hiyo ya Chopa. 

"Kwa masikitiko makubwa nimepokea taarifa rasmi kutoka kwa timu ya uokoaji kuwa imefanikiwa kufika eneo la ajali na kukuta abiria wote na rubani wamepoteza maisha.
"Ni mepoteza Baba na rubani mzuri wa nchi yetu Capt. William Silaa.
 Nimepoteza rafiki na kiongozi wangu Mhe. Deo Filikunjombe. Nawapa pole wote waliopoteza ndugu zao. Nawaombea marehemu mapumziko ya Amani. Nawashukuru wote walioshirikiana na familia kusaidia uokozi", amesema Mhe Jerry Silaa katika kurasa zake za mitandaoni.
Tangia jana habari za kuanguka kwa chopa hiyo zilitapakaa kila kona na katika mitandao, na kuendelea hadi jana tangia asubuhi hadi baada ya ujumbe wa Jerry Silaa kupatikana mchana wa jana.

Comments