Monday, October 26, 2015

RAIS KIKWETE AMTEUA MKURUGENZI MKUU WA TAASISI YA TEA

Laurent

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TEA), Ndugu Joel Laurent.TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Ndugu Joel Laurent kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TEA).
Uteuzi huo ulianza Oktoba 18, mwaka huu, 2015. Kabla ya uteuzi wake, Ndugu Laurent alikuwa Katibu wa Taasisi hiyo ya TEA na ndiye amekuwa anakaimu nafasi ya Mkurugenzi Mkuu.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu, DAR ES SALAAM.
26 Oktoba, 2015.

No comments:

RAIS DKT. SAMIA AKUTANA NA UJUMBE WA JUKWAA LA MABUNGE LA NCHI ZA MAZIWA MAKUU (FP-ICGLR) IKULU NDOGO TUNGUU, ZANZIBAR

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Kiongozi wa Jukwaa la Mabunge la...