UNICEF YAKABIDHI MAGARI KUMI( 10) YA KUBEBEA WAGONJWA MKOANI MBEYA

New Picture (1)
Mratibu wa Huduma za Afya ya Uzazi na Mtoto Ndugu Prisca Butuyuyu akitoa taarifa ya huduma za Afya ya Uzazi na Mtoto katika Mkoa wa Mbeya kwenye hafla fupi ya makabidhiano ya magari ya kubebea wagonjwa 15 Octobar 2015.
New Picture (5)
Kastro Msigala Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mbeya ambaye alikuwa mgeni rasmi katika sherehe hizo za makabidhiano ya magari kumi ya kubebea wagonjwa ambayo yametolewa na shirika la kimataifa la UNICEF Octobar 15 mwaka huu.
New Picture
Mwakilishi wa Shirika la Kimataifa la Unicef Dkt Jama Gulaid akitoa hotuba katika sherehe ya makabidhiano ya magari ya kubebea wagonjwa Mkoa wa Mbeya15 Octobar 2015
New Picture (6)
Kaimu Katibu tawala Mkoa wa Mbeya Kastro Msigala akikata utepe kuashiria kupokea rasmi msaada wa magari hayo kutoka kwa shirika la kimataifa la UNICEF msaada ambao umegharimu kiasi cha shilingi Mil 700.
New Picture (2)
Mwakilishi UNICEF Dkt Jama Gulaid kulia akimkabidhi Kaimu katibu Tawala Mkoa wa Mbeya Ndugu Kastro Msigala taarifa muhimu za magari hayo yenye thamani ya shilingi mil 700 .
New Picture (3)
Viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Mbeya pamoja na wageni waalikwa wakishiriki kikamilifu tukio la makabidhiano ya magari ya wagonjwa Mkoa wa Mbeya 15 Octobar 2015 kutoka kwa shirika la kimataifa la UNICEF.
New Picture (4)
Timu ya Uendeshaji wa huduma za za Afya Mkoa wa Mbeya.
   New Picture (7)
Meza kuu katika picha ya pamoja na viongozi wa Mkoa wa Mbeya na wawakilishi wa Shirika la UNICEF.
New Picture (8)
Meza kuu katika picha ya pamoja na waganga wakuu wa Halmashauri za Mkoa wa mbeya .
………………………………………………………….
SHIRIKA la Umoja wa Mataifa linalo shughulikia
watoto Duniani (UNICEF) limekabidhi msaada wa magari kumi ya Kubebea wagonjwa yenye tahamni ya shilingi
mil 700.7 kwa serikali ya Mkoa wa Mbeya .
Aidha shirika hilo lina mpango wa kuboresha vituo 184 vya kutolea huduma za afya
katika mkoa huo wa mbeya ambavyo ni vituo afya na hospital 30 pamoja na
zahanati 154 sanjali na kuvipatia vifaa
muhimu vya kutolea mafunzo kwa watumishi wake.
Akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika katika ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Octobar 15
mwaka huu Mwakilishi wa shirika la UNICEF 
nchini Tanzania Dkt Jama Gulaid amesema
shirika hilo limetenga kiasi cha shilingi bilioni 2 kwa ajili ya mradi huo.
Amesema mchango wa UNICEF katika sekta afya na lishe hapa mkoani mbeya imepanua wigo
kutoka halmashauri mbili za mkoa huo hadi kufikia halmashauri zote katika
kipindi cha miaka miwili .
Aidha Dtk, Jama amesema katika kukabiliana na magonjwa na vifo vya watoto na wanawake
wajawazito ,UNICEF imechangia vifaa tiba muhimu ikiwa ni pamoja vile vya uchunguzi
wa ujauzito ,upasuaji sanjali na vifaa
kuwasaidia watoto wachanga kupumua mara wanapo zaliwa na vifaa vingine vya
utoaji wa huduma katika idara ya uangalizi maalumu ICU.
Aidha amewataka viongozi hao wa mkoa wa Mbeya
kuhakikisha wanaweka juhudi kubwa zaidi katika kupunguza vifo vya akina mama na
watoto wachanga kwa kuhakikisha kwamaba kina mama wajawazito wote wanapata
huduma za afya bure kwa wakati.
Awali akisoma taarifa ya huduma za afya ya
uzazi na mtoto katika mkoa mbeya mratibu wa huduma za afya ya uzazi na mtoto
Ndugu Prisca Butuyuyu amesema toka
shirika hilo la UNICEF lianze kufanya
mwaka 2012 huduma za afya zimeimalika kwa kiasi kikubwa hususani kwa kuweza
kuzuia vifo vya uzazi na vya watoto wachanga.
Amesema kwa ujumla hali ya vifo hususani vilivyokuwa 
vinatokea katika vituo vya huduma vimepungua kutoka 140 kwa mwaka 2012 na kufikia vifo 94 kwa kwa
mwaka 2014 pamoja na kupunguza vifo vya watoto wachanga kutoka 602 kwa mwaka
2012 hadi kufikia 568 mwaka 2014 ambapo punguzo
hilo ni sawa na asilimia 33.9 na 5.7 kwa watoto wachanga.
Akipokea msaada huo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Kaimu katibu Tawala Ndugu Kastro
Msigala amelishukuru shirika hilo kwa msaada wa magari hayo sanjali na kutoa
wito kwa viongozi wa halmashauri ambao
ni wakurugenzi na waganga wakuu kuhakikisha wanayatunza magari hayo ili yaweze
kutoa huduma stahiki kwa wananchi.
Msaada huo wa magari imegawanywa katika halmashauri zote mkoa huo wa mbeya ambazo ni
Ileje,Mbozi,Mbeya vijijini,Rungwe,Busokelo,Mbarali pamoja na Kyela na Momba .
(Imeandaliwa na
Jamiimojablog Kanda ya Nyanda za juu kusini Mbeya.

Comments