Monday, October 05, 2015

ZIARA YA KATIBU MKUU WA WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA BALOZI LIBERATA MULAMULA KATIKA OFISI YA UBALOZI WA TANZANIA OTTAWA-CANADA, OKTOBA 1-3, 2015

 Mhe.  Balozi Liberata Mulamula, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akiwasili kwenye Ofisi za Ubalozi wa Tanzania, Ottawa – Canada, akiongozana na mwenyeji wake Mhe. Balozi Jack M.  Zoka, tayari kuanza kazi alizozipanga kufanya katika ziara hiyo.
 Mhe. Balozi Liberata Mulamula akisaini kitabu cha wageni hapo Ubalozini. Pembeni ni mwenyeji wake Mhe. Balozi M.  Zoka.
 Picha ya Pamoja ya wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania Ottawa na Mhe. Katibu Mkuu, Balozi Liberata Mulamula, aliyesimama katikati, kushoto kwa Balozi Jack M. Zoka; Kutoka kulia ni Bw. Paul Makelele, Bibi Nsia Paul na kutoka kushoto ni Bibi Aziza Bukuku akifuatiwa na Bw. Richard Masalu.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Balozi Liberata Mulamula, akisoma maandishi yaliyomo kwenye sovenia aliyoandaliwa na Kamati ya Maandalizi ya Ziara yake katika Ofisi ya  Ubalozi ya Tanzania Ottawa, Canada.

 Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Balozi Liberata Mulamula akiagana na wenyeji wake katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa, Ottawa, mara baada ya kukamilisha Ziara yake ya Kikazi Ubalozini, Ottawa – Canada
Post a Comment