Thursday, October 29, 2015

SAFU MPYA YA MAKATIBU NA NAIBU MAKATIBU WAKUU NISHATI NA MADINI YAKABIDHIWA OFISI

ch1

Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi (kulia), akibadilishana Nyaraka za Makabidhiano na Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Omari Chambo (Kushoto). Maswi ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara.
ch2
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Omari Chambo (Kushoto), akisaini Nyaraka za Makabidhiano sambamba na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Manyara.
ch6

ch5
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Paul Masanja (kulia) akipokea shada la maua kutoka kwa Cecilia Mrope Afisa kutoka Wizara ya Nishati na Madini.
ch4
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Omari Chambo, akiongea jambo na Wajumbe wa Menejimnenti wa Wizara baada ya kuwasili wizarani hapo. Katibu Mkuu alitumia kikaohicho kuwaeleza wajumbe masuala muhimu ambayo atayasimamia kikamilifu katika sekta za Nishati na Madini.
ch3Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi akimpongeza, aliyekuwa Kamishna wa Madini Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi
…………………………………………………………………………….
  • Makatibu wapya wataja vipaumbele
  • Kuzingatia 4Us, Uendelezaji Wachimbaji Wadogo
Teresia Mhagama na Asteria Muhozya
Katibu Mkuu mpya na Naibu Katibu Mkuu  walioteuliwa kuiongoza Wizara ya Nishati na Madini wameanza majukumu yao na kusisitiza watumishi wa Wizara na Taasisi zake kuzingatia Uadilifu, Ubunifu, Uwajibikaji, na Uwazi katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.
Wakizungumza  na wajumbe  wa menejimenti ya Wizara ya Nishati na Madini, viongozi hao walisisitiza  baadhi ya masuala yatakuwa  kipaumbele  kuwa ni uwepo wa umeme wa uhakika na bei nafuu ili wananchi watumie nishati hiyo kujiletea maendeleo na kukuza uchumi wa nchi.
Vipaumbele vingine ni kuongeza mchango wa sekta madini katika pato la Taifa, uwepo wa kiwanda cha kusindika gesi asilia, na suala la uwezeshaji wazawa(Local Content) katika sekta za Nishati na Madini.
Vilevile, vipaumbele vingine ni kuhakikisha kuwa wachimbaji wadogo wanasaidiwa katika masuala ya fedha na utaalam na kuboresha mazingira na maslahi ya wafanyakazi.
Katibu Mkuu, Mhandisi Omari Chambo, pamoja na kumshukuru aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi kwa kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi mkubwa, alitoa wito wa ushirikiano kati ya uongozi huo mpya na wafanyakazi.
Naye, Naibu Katibu Mkuu, Mhandisi Paul Masanja pamoja na kuainisha vipaumbele mbalimbali  vya utekelezaji amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete kwa kumteua kushika nafasi hiyo   na kueleza kuwa, imetokana na kuridhika na utendaji wake wa kazi wakati aliposhika nyadhifa mbalimbali ikiwemo kuwa Kamishna wa Madini nchini.
Alitoa wito kwa wafanyakazi wa Wizara ya Nishati na Madini kutoa ushirikiano kwa uongozi huo ili kwa pamoja waweze kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazojitokeza katka uendelezaji wa sekta za Nishati na Madini.
Kabla ya kukabidhi nyaraka za makabidhiano, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Nishati na Madini, Eliakim Maswi  ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara, aliwashukuru watumishi wa Wizara ya Nishati na Madini kwa ushirikiano waliompa wakati wa kipindi cha uongozi wake na kuwaasa kufanya kazi kwa bidii na kutoa ushirikiano kwa uongozi mpya.
Vilevile, aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu, Mhandisi Ngosi Mwihava ambaye ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji, aliwaasa Watumishi kuendelea kufanya kazi kwa kushirikiana, kuzingatia taratibu, sheria na kanuni, kuzingatia muda na kuimarisha mawasiliano.
Kabla ya kushika nyadhifa hizi Katibu Mkuu, Mhandisi Omari Chambo alikuwa Katibu Tawala mkoa wa Manyara na Naibu Katibu Mkuu, Mhandisi Paul Masanja alikuwa Kamishna wa Madini nchini.
Post a Comment