Thursday, October 22, 2015

WANANCHI WAMESEMA COSATO CHUMI KUIJENGA MAFINGA MPYA AKIPEWA RIDHAA

Mgombea ubunge wa jimbo hili kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Cosato akiwahutubia wananchi wa Ihimbo
Chalamila kampeni meneja akihutubia wanachi wa Ihimbo
Mgombea ubunge wa jimbo hili kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Cosato akiongea na mlemavu wa viungo kwenye mkutano wa Ihimbo.
……………………………………
Na fredy Mgunda, Mafinga

Wananchi wa kata ya rungemba katika jimbo la mafinga
mjini wampongeza mgombea ubunge wa jimbo hili kupitia tiketi ya chama cha
mapinduzi (CCM) cosato chumi kwa kufanya kampeni za kistaarabu na kuwapa
matumaini kuwa atakuwa kiongozi mzuri na kuwaletea maendeleo katika jimbo hilo.
“Tumeona wagombea wengi wakija hapa kupiga kampeni na
kuomba kura kwa njia ya matusi na kuhamasisha kutomchagua kiongozi furani
pasipo kutaja au kuongelea hata hoja za msingi kwanini wanaomba kura zetu”
walisema wananchi hao
Waliongeza kwa kusema kuwa imefika wakati wananchi
wanapaswa kuwakata wapinzani katika jimbo hilo kutokana tabia yao kuwafundisha
tabia mbaya wafuasi wao hasa wanapoamua kuanza kuchana mabango ya wagombea wa
chama cha mapinduzi (CCM)
“Tuliwakamata baadhi ya vijana wakiwa wananchana
mabango ya wagombea wa ccm katika kata hii lakini tulipowafikisha kituo cha
polisi walisema wanatumwa na viongozi wa chama cha demokrasia na maendeleo
chadema” walisema wananchi hao
Wananchi hao wamewasisitia wananchi wa jimbo hilo kutunza
na kuhifadhisehemu nzuri vitambulisho vyao vya kupigia kura kutokana na tabia
inayoanza hivi sasa wanataka namba za vitambulisho na wengine wananunua
vitambulisho hivyo wananchi tutajinyia haki yetu ya msingi ya kumchagua
kiongozi tunayemtaka kwa kuza vitambulisho vyetu.
“Kwa sasa wananpita usiku waki wakitaka kununua
vitambulisho vyenu au tuwatajie namba za vitambulisho vyenu na kuahidi kutupa
kiasi kikubwa cha pesa ili kufanikisha lengo lao,hivyo tunawaomba jeshi la
polisi na mamlaka husika kulizibiti tatizo hilo kabla ya uchaguzi ili wananchi
watumie haki yao ya msingi”.walisema wananchi hao
Kwa upande wake mgombea ubunge wa jimbo hilo kupitia
chama cha mapindizi (CCM) COSATO CHUMI amesema wananchi wanapashwa kuwa makini
na mbinu chafu zinazotumiwa na wapinzani wake kwa kuwalaghai wananchi kwa
kununua vitambulisho au kunakili namba za vitambulisho hivyo
.
“Tuwakatae viongozi wa namna hiyo kwa kuwa lengo lao
ni kutaka kuununua uongozi kwa nguvu ya pesa na kuwa wao sio chaguo la wanachi
hivyo wananchi msidhubutu kufanya hivyo mtapoze haki yenu ya msingi na hampata
kiongozi atakaye waletea maendeleo”.alisema chumi
Lakini chumi alisikika akiwaambia wananchi wa kata
hiyo tuwakatae wagombea hao wanaohamasisha kuturushia mawe kwenye mikutano yenu
lakini kupiga mawe gari zenu na kuhamasisha vurugu kwa wananchi katika kipindi
hiki cha kampeni je mkiwapa madaraka si ndio watawaongoza kwa kutumia mabavu
kwa kuwa hata kuingia madarakani wametumia nguvu.
“Nawaombeni wanachi wa kata ya rungemba kukipigia kura
cha chama cha mapinduzi (CCM) kuanzia ngazi ya udiwani,ubunge hadi urais kwa
kuwa viongozi hao wote wanasifa ya kuwa viongozi wa nchi hii”alisema chumi.
Naye kampeni meneja wa mgombea huyo amewataka wananchi
kuwataa kabisa wapinzani kwa kuwa si waadilifu kutokana na wazazi wao
kujilimbikizia mali kipindi baba yake akiwa mbunge kwa takribani miaka
thelathini  na sasa wanatumia mali hizo
kuwadanganya wananchi na kuwaraghai kwa vijipesa vyao lakini wao hawana aiba ya
kuwa viongozi.
Alimalizia kwa kuwaomba wananchi wa jimbo hilo
kumchagua cosato chumi kwa kuwa ni kiongozi mzuri na atawaletea maendeleo
wananchi wa jimbo hilo. 
Post a Comment