Naibu Katibu Mkuu Mpya wa Wizara ya Mawasiliano Sayansi na Teknolojia Ndugu Emannuel Kalobelo akila kiapo mbele ya Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dar es salaam Oktoba 26, 2015.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete amewaapisha manaibu katibu wawili wa wizara na Katibu Tawala wa mkoa katika hafla fupi iliyofanyika ikulu jijini Dar es Salaam Oktoba 26, 2015.Manaibu katibu walioapishwa ni pamoja Ndugu Emmanuel Kalobelo anayekuwa Naibu Katibu mkuu Wizara ya Mawasiliano Sayansi na Teknolojia na ndugu Tixon Nzunda nayekuwa Naibu Katibu Mkuu,Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma.
Katika hafla hiyo Rais Kikwete amemwapisha Mhandisi Madeni kipande kuwa katibu Tawala wa mkoa wa Katavi .
Katika hafla hiyo Rais Kikwete amemwapisha Mhandisi Madeni kipande kuwa katibu Tawala wa mkoa wa Katavi .
Naibu Katibu Mkuu mpya Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Ndugu Tixon Nzunda akila kiapo mbele ya Rais Kikwete.
Katibu Tawala mpya wa mkoa wa Katavi Mhandisi Madeni Kipande akila kiapo mbele ya Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dar es salaam leo na kukabidhiwa miongozo ya kazi.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue(wapili kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na waliapishwa leo.Kushoto ni Katbu Tawala Mkoa wa Katavi Ndugu Madeni kipande, wanne kushoto ni Naibu katibu Mkuu mpya wa Wizara ya Mawasiliano Sayansi na Teknolojia Ndugu Emmanuel Kalobelo na kulia ni Naibu Katibu Mkuu Mpya Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma Ndugu Tixon Nzunda.
Picha na Freddy Maro
Comments