Friday, October 23, 2015

WAANGALIZI WA UCHAGUZI KUTOKA UMOJA WA AFRIKA (AU) WAMTEMBELEA WAZIRI CHIKAWE OFISINI KWAKE

 1
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (kushoto) akimkaribisha ofisini kwake Mkuu wa Timu ya Waangalizi wa Uchaguzi Mkuu Tanzania kutoka Umoja wa Afrika (AU), Rais wa Zamani wa Msumbiji, Mhe Armando Emilio Guebuza.
2
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias Chikawe (Katikati kulia) akimfafanulia jambo Mkuu wa Timu ya Waangalizi wa Uchaguzi Mkuu Tanzania kutoka Umoja wa Afrika (AU), Rais wa Zamani wa Msumbiji, Mhe Armando Emilio Guebuza (wapili kushoto), pamoja na wajumbe wenzake, jinsi Tanzania ilivyojipanga kuhakikisha Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu utakavyokuwa wa amani. Wakwanza kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mbarak Abdulwakil.
3
Mkuu wa Timu ya Waangalizi wa Uchaguzi Mkuu Tanzania kutoka Umoja wa Afrika (AU), ambaye pia ni Rais wa Zamani wa Msumbiji, Armando Emilio Guebuza (kulia) akimfafanulia jambo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (kushoto) wakati Mkuu huyo pamoja na wajumbe wenzake walipomtembelea Waziri Chikawe ofisini kwake kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali ya Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu, hata hivyo, Chikawe aliwahakikishia kuwa Uchaguzi huo utakuwa wa amani. Wapili kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mbarak Abdulwakil.
Picha zote na Felix Mwagara, 

No comments:

RAIS SAMlA AFANYA MAZUNGUMZO NA MJUMBE MAALUM WA RAIS TSHISEKEDI

  Dar es Salaam, 26 Machi 2025 – Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan , amekutana na kufanya mazungu...