MCHAKAMCHAKA WA MWIGULU MKOANI MBEYA, AINADI CCM TUNDUMA, KYELA,UYOLE

Mwigulu Nchemba akisalimiana na Wananchi wa Mji wa Tunduma asubuhi ya jana alipokwenda kuomba kura za Rais, Ubunge na Madiwani wa Chama cha Mapinduzi.
“Watanzania wenzangu mnaoishi hapa Tunduma, Hakuna chama cha siasa chenye thamani kuliko UHAI wa Mwanadamu, Nawaombeni sana muache tabia za kupigana na kuuana kwasababu ya vyama vya siasa. Nyie wananchi mnagombana kwa sababu ya siasa, Hivi ni lini mmeona sisi viongozi wa vyama vya siasa tunapigana??” Mwigulu Nchemba.
Wananchi wa Tunduma wakishangilia hoja za Mwigulu Nchemba kuhusu Uadui wa vyama vya siasa na Uongozi wanaokwenda kuuchagua.
Furaha ya WanaCCM wanapothibitishiwa Usalama wao wakati wa kwenda kupiga kura hapo October 25.
“CCM tumefanya hesabu kwenye Uchaguzi huu na hesabu imekubali,Magufuli anakwenda kushinda Uchaguzi huu.Mgombea wa CCM hadi sasa anawazidi wagombea wengine kwa Uadilifu,Ubora wa sera zake,rekodi yake ya Uchapakazi lakini ni Mzalendo kwa Taifa lake”Mwigulu akizungumza na wananchi wa Tunduma hii jana.
Mwigulu akimnadi Mgombea Ubunge Ndg.Frank wa Chama cha Mapinduzi wakati wa mkutano huo.
“Twendeni tukaichague CCM,Chama chenye Dira ya maendeleo ya kweli wa Watanzania,hao wengine wangekuwa wanmabadiliko wangeyafanya wakati walipokuwa serikalini,Hivi sasa hawana nafasi tena”
Umati wa Wananchi wa Mji wa Tunduma wakiendelea kusikiliza Mkutano wa Mwigulu Nchemba mapema hii jana asubuhi.
Kura za wazi wa Magufuli kutoka kwa Wananchi wa Tunduma walipoulizwa na Mwigulu Nchemba watakao mpigia kura Magufuli wainue mikono yao.
Wananchi wakifuatilia mkutano kwa makini tayari kwa kufanya maamuzi ya kuipigia kura CCM.
Makada wa tiifu wa Chama cha Mapinduzi wakikutana hii jana Kyela.Ni Dr.Harrison Mwakyembe na Mwigulu Nchemba.
Hisia za Wanakyela wanapoambiwa Nchi nzima wanaimba Magufuli, Hivyo hakuna shaka juu ya Ushindi wake.
“Twende na Magufuli,tunataka kazi tu”
Mwigulu Nchemba akizungumza na Wananchi wa kata ya Nzovwe jioni ya jana.
“Vijana wenzangu wa Uyole, Maendeleo hayaji kwa kupiga Rami deki ili mtu ambaye Upinzani kwa miaka Zaidi ya 10 walikuwa wanamuita Mwizi, Maendeleo yanakuja kwa mipango. Msipandikizwe chuki juu ya CCM, wakati watendaji wa serikali hawaajiliwi kwa kadi za CCM na wengine wapo serikalini hawana hata urafiki na CCM. Hivyo basi tumewaletea Magufuli abadilishe utendaji serikalini na sio vyama vya siasa”.
Mwigulu Nchemba akizungumza na wananchi wa kata ya Uyole hii jana Jioni.
WanaCCM wakishangilia hoja za Mwigulu Nchemba.
Wananchi wa Uyole(Junction)wakimsindikiza Mwigulu Nchemba kwenda kupanda Gari mara baada ya Mkutano wa hadhara wa kumuombea kura Magufuli,Diwani na Mbunge wa CCM.
Picha na Sanga Festo Jr.

Comments