Sunday, October 25, 2015

RAIS JAKAYA KIKWETE AWAAPISHA MAKATIBU WAKUU

 x2

Dkt.Maria Mashingo akila kiapo mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Kikwete baada ya kuteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Ikulu  jijini Dar es Salaam Oktoba 24, 2015.
x3
Prof.Elisante Gabriel akila kiapo mbele  ya Rais wa Jamhuri ya Muungano  Dkt. Jakaya Kikwete baada ya kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo,  Ikulu  jijini Dar es Salaam Oktoba 24, 2015,awali Prof.Gabriel alikuwa Naibu Mkuu wa Wizara hiyo.
x4
Rais wa Jamhuri ya Muungano  Dkt.Jakaya Kikwete akimpongeza Bw.Eliakim Maswi mara baada ya kumaliza kula kiapo Ikulu jijini Dar es salaam,Bw.Maswi ameteuliwa kuwa  Katibu Tawala Mkoa wa Manyara.
x5
Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Prof.Elisante Gabriel (katikati)akipongezwa na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bibi Sihaba Nkinga (kulia) ambaye amehamishiwa Wizara ya Wanawake,Jinsia na Watoto pamoja na Msemaji Mkuu wa Serikali Bw.Assah Mwambene (Kushoto),mara baada ya kuapishwa   Ikulu jijini Dar es Salaam.
x6
Rais wa Jamhuri ya Muungano  wa Tanzania Dkt.Jakaya Kikwete(Kulia) akiwa katika picha na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo,Chakula na Ushirika Bw.Zidikheri Mundeme  mara baada ya kuapishwa ikulu jijini Dar es Salaam.
x7
Rais wa Jamhuri ya Muungano  wa Tanzania Dkt.Jakaya Kikwete(kulia) akiwa katika picha na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw.Hab Mkwizu mara baada ya kuapishwa  ikulu jijini Dar es Salaam.
x1
Rais wa Jamhuri ya Muungano  wa Tanzania Dkt.Jakaya Kikwete (watano kulia) pamoja na Katibu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue (watano kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na Makatibu Wakuu waliyoteuliwa mara baada ya kuapishwa  Ikulu Jijini Dar es Salaam Oktoba 24,2015.
Picha zote na Anitha Jonas – MAELEZO.
Post a Comment