Wednesday, October 21, 2015

LOWASSA AONGOZA MAMIA KUUAGA MWILI WA DK.EMMANUEL MAKAIDI VIWANJA VYA KARIMJEE DAR ES SALAAM

Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kupitia mwamvuli wa Ukawa, Edward Lowassa akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti Mwenza wa umoja huo, Dk. Emmanuel Makaidi wakati wa ibada ya kuuaga iliyofanyika viwanja vya Karimjee Dar es Salaam jana mchana. Katika ibada hiyo viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa na serikali walihudhuria.
Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye ibada hiyo.
Wananchi wakiwa wamejipanga foleni wakati wakienda kutoa heshima za mwisho kwa marehemu.
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Tanzania Bara, Philip Mangula (kulia), akipeana mkono wa pole na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe wakati alipofika kuhudhuria ibada hiyo.
Mjane wa marehemu, Dk. Emmanuel Makaidi, Modesta Ponela akiwa ameinua mikono wakati akimuaga mumewe katika ibada hiyo
Msajili wa Vyama Vya Siasa, Jaji Francis Mtungi, akizungumza kwa niaba ya serikali wakati wa misa hiyo ya kumuaga Dk. Makaidi.

No comments:

RAIS DKT. SAMIA AKUTANA NA UJUMBE WA JUKWAA LA MABUNGE LA NCHI ZA MAZIWA MAKUU (FP-ICGLR) IKULU NDOGO TUNGUU, ZANZIBAR

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Kiongozi wa Jukwaa la Mabunge la...