DK. JOHN POMBE MAGUFULI AUNGURUMA JANGWANI, ATOA HOTUBA KALI KWA WANAOBEZA MIAKA 54 YA MAFANIKIO YA SERKIALI
Posted by
Vempin Media Tanzania
on
- Get link
- X
- Other Apps
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Kikwete akimnadi Mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dk. John Pombe Magufuli kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye viwanja vya Jangwani leo jijini Dar es salaam huku akiwaomba watanzania na wana CCM kokote waliko nchini kumpigia kura za ndiyo mgombea huyo siku ya jumapili Oktoba 25 mwaka huu ili aweze kuwatumikia kwa uadilifu, uaminifu na kuwaletea maendeleo ya kiuchumi na kijamii watanzania kwa ujumla wao.
Dk. Kikwete amemuelezea Dk. Magufuli kuwa ni mwadilifu, Mnyenyekevu, Mzalendo, Mchapakazi na anawapenda watanzania wote kwa ujumla wake hivyo watanzania hawana budi kumpa kura za ndiyo ili awe rais wa Tanzania na kuiletea maendeleo nchi na watanzania kwa ujumla.
Naye Dk. John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi waliojitokeza kwa wingi katika mkutano huo amesema kuna baadhi ya watu wanasema miaka 54 iliyopita Serikali haijafanya lolote jambo ambalo ni upotoshaji jamii wa kiwango cha hali ya juu, Watu hao walikuwa ni viongozi wakubwa katika serikali na walimshauri rais kwa mambo mengi ya kiutendaji serikalini.
Ni jambo la ajabu watu waliowahi kuwa na madaraka makubwa serikalini leo wanasema hakuna jambo lolote lililofanyika kwa miaka 54 ya uhuru wetu, Je muda wote walikuwa wapi si wangeondoka mapema ili ijulikane moja, Dk. Magufuli ameongeza na kusema serikali zote kuanzia ya awamu ya kwanza mpaka ya nne zimefanya mambo mengi mazuri na zinastahili kupongezwa kwa sababu hata hii amani tuliyonayo Mwalimu J.K.Nyerere alifanya kazi kubwa kuwaunganisha watanzania makabila zaidi ya 120 na kuwa kitu kimoja.(PICHA NA JOHN BUKUKU-JANGWANI DAR ES SALAAM)
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Kikwete akikumbatiana na Mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dk. John Pombe Magufuli kwa furaha, kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye viwanja vya Jangwani jijini Dar es salaam wakati akimkaribisha ili aweze kuwahutubia wananchi waliohudhuria katika mkutano huo.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Kikwete akiwahutubia wananchi katika mkutano huo.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Kikwete akisisitiza jambo wakati akihutubia katika mkutano huo.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kikwete akimkaribisha Dk. John Pombe Magufuli ili kuhutubia mkutano huo kwenye viwanja vya Jangwani.
Mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia katika mkutano huo uliofanyika viwanja vya Jangwani jijini Dar es salaam .
Mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dk. John Pombe Magufuli akisisitiza jambo wakati akihutubia katika mkutano huo uliofanyika viwanja vya Jangwani jijini Dar es salaam .
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Kikwete Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wa pili kutoka kulia, Makamu Mwenyekiti wa CCM Mzee Philip Mangula wa kwanza kushoto na Mama Salma Kikwete wakifurahia jambo wakati Dk. John Pombe Magufuli hayupo pichani akitoa hotuba yake katika mkutano huo.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Kikwete akimkaibisha Mama Janeth Magufuli ili amuombee kura mume wake Dk. John Pombe Magufuli.
Mama Janeth Magufuli akimpigia debe na kumuombea kura mume wake Dk. John Pombe Magufuli katika mkutano huo.
Mama Salma Kikwete akizungumza katika mkutano huo ambapo amewashukuru watanzania kwa kumuamini mume wake Rais Dk.Kikwete kuwaongoza watanzania kwa muda wa miaka 10 kama kiongozi mkuu wa Taifa la Tanzania.
Umati mkubwa ukiwa katika mkutano huo.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Kikwete na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakionekana wenye furaha wakati Dk. John Pombe Magufuli alipokuwa akiwahutubia wananchi katika mkutano huo, kutoka kulia ni Mama Janeth Magufuli na Mama Salma Kikwete.
Kutoka kushoto ni Ndugu Abdulrahman Kinana, Mama Salma kikwete, Mama Janeth Magufuli na Mama Zakhia Megji wakicheza nyimbo za hamasa zilizokuwa zikitumbuizwa na kundi la muziki la TOT.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Kikwete akimnadi mgombea ubunge wa jimbo la Kigamboni Dk. Faustine Ndungulile.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Kikwete akimnadi mgombea ubunge wa jimbo la Ukonga Ndugu Jerry Silaa.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Kikwete akimnadi mgombea ubunge wa jimbo la Kawe Ndugu Kipi Warioba.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wanachi katika mkutano huo
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Kikwete akizungumza na Dk. John Pombe Magufuli wakati mkutano huo ukiendelea.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Kikwete akiwasili kwenye viwanja vya jamngwani kwa ajili ya mkutano huo wa kampeni kulia ni Dk. John Pombe Magufuli mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM na kushoto ni Ndugu Abdulrahman Kinana Katibu Mkuu wa CCM.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Kikwete akisalimiana na Dk. John Pombe Magufuli wakati alipowasili kwenye viwanja vya Jangwani kwa ajili ya mkutano wa kampeni wa CCM kushoto ni Ndugu Abdulrahman Kinana Katibu Mkuu wa CCM.
Vituko vya kampeni havikosi.
Msanii Ali Kiba akifanya vitu vyake katika mkutano huo.
Mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dk. John Pombe Magufuli akipungia mkono wananchi wakati alipowasili kwenye viwanja vya Jangwani.
Nyami ya wananchi kama inavyoonekana kwenye picha.
Abdul Nassib Diamond Platnumz naye akafanya mambo makubwa katika mkutano huo.
PICHA ZOTE ZA BASHIR NKOROMO BLOG
Comments