Friday, October 23, 2015

DK. JOHN POMBE MAGUFULI: NIKIINGIA MADARAKANI SERIKALI YANGU HAKUNA MICHAKATO WALA CHANGAMOTO “HAPA NI KAZI TU”

????????????????????????????????????
 Dk. John Pombe Magufuli Mgombea Urais kupitia CCM akiwahutubia wakazi wa jiji la Dar es salaam jimbo la Kawe katika mkutano uliofanyika Bunju jana. 
Dk John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi hao waliojitokeza kwa wingi ili kumsikiliza amewaomba kumpigia kura za ndiyo Oktoba 25 jumapili mwaka huu katika uchaguzi wa Rais , Wabunge na Madiwani ili awe rais na kuwatumikia watanzania kwa kuleta maendeleo ya kiuchumi kwa watanzania kwa ujumla wake.
Dk. Magufuli amesema mara atakapoingia madarakani serikali yake itakuwa ya kufanya kazi zaidi na kuwajibika kwa watanzania ambao wamekuwa wakilalamika mara nyingi juu ya utendaji wa baadhi ya watendaji wa serikali ambao hawawawajibika ipasavyo kwa taifa jambo ambalo linapelekea tija ya utendaji kushuka serikalini kwa sababu ya utendaji wa Michakato, “Serkali yangu haitakuwa ya Michakato au Changamoto Mimi kwangu ni Kazi Tu”
Mgombea huyo amefanya mikutano yake ya kampeni katika majimbo ya  Kibaha Vijijini, Chalinze, Kibaha mkoani Pwani pia amefanya mikutano  Kibamba na Kawe mkoa wa Dar es salaam (PICHA NA JOHN BUKUKU-BUNJU DAR ES SALAAM)
????????????????????????????????????
 Dk. John Pombe Magufuli Mgombea Urais kupitia CCM akisisitiza jambo wakati alipokuwa akihutubia mkutano wa kampeni Bunju jimbo la Kawe.
????????????????????????????????????
Jaji Joseph Warioba akimpigia debe Dk John Pombe Magufuli kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika Bunju jimbo la Kawe.
????????????????????????????????????
Makamu wa Rais na Mjumbe wa Kamati kuu ya CCM Dk Gharib Bilal akimpigia debe Dk. John Pombe Magufuli katika mkutano huo.
????????????????????????????????????
Baadhi ya wananchi wakiwa juu ya paa la nyumba wakimsikiliza Dk. John Pombe Magufuli.
????????????????????????????????????
Mgombea ubunge wa jimbo la Kawe Kipi Warioba akiwaomba kura wananchi wa jimbo lake la kawe katika mkutano wa kampeni uliofanyika Bunju jijini Dar es Salaam.
????????????????????????????????????
Maelfu ya wananchi wakiwa katika mkutano huo.
????????????????????????????????????
????????????????????????????????????
????????????????????????????????????
????????????????????????????????????
Baadhi ya viongozi wakiwa katika jukwaa kuu wakati mkutano huo ukiendelea.
????????????????????????????????????
 Dk. John Pombe Magufuli Mgombea Urais kupitia CCM akimnadi mgombea ubunge wa jimbo la Kawe Ndugu Kipi Warioba na kumkabidhi ilani ya uchaguzi ya CCM.
????????????????????????????????????
 Dk. John Pombe Magufuli Mgombea Urais kupitia CCM akimnadi mgombea ubunge wa jimbo la Kawe Kipi Warioba.
????????????????????????????????????
 Dk. John Pombe Magufuli Mgombea Urais kupitia CCM akisalimana na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Sar es salaam Ndugu Ramadhan Madabida  wa tatu kutoka kulia ni  Makamu wa Rais Dk Gharib Bilal wakati alipowasili kwenye uwanja wa mkutano huo uliofanyika Bunju jimbo la Kawe jijini Dar es salaam kutoka kulia ni Dk. Fennela Mukangara mgombea ubunge jimbo la Kibamba na Mgombea ubunge jimbo la Kawe,
????????????????????????????????????
Dk. John Pombe Magufuli Mgombea Urais kupitia CCM akisalimana na Makamu wa Rais Dk Gharib Bilal wakati alipowasili kwenye uwanja wa mkutano huo uliofanyika Bunju jimbo la Kawe jijini Dar es salaam.
????????????????????????????????????
Dk. John Pombe Magufuli Mgombea Urais kupitia CCM akishangilia wana wanachama wa Chadema wakati alipowaomba kura aliposimama Tegeta wakati akiwa njiani kuelekea Bunju  jijini Dar es salaam kwa ajili ya kufanya mkutano wa kampeni. 
????????????????????????????????????
Dk. John Pombe Magufuli Mgombea Urais kupitia CCM akishangiliwa na wana Chadema.
????????????????????????????????????
Bendera mbalimbali za Chadema na CCM zikiwa zimepambwa mitaani jijini Dar es salaam.
????????????????????????????????????
Dk. John Pombe Magufuli Mgombea Urais kupitia CCM akimnadi mgombea ubunge wa jimbo la Kibaha mjini Mh Sylivester Koka katika mkutano uliofanyika maili moja mjini Kibaha leo.
????????????????????????????????????
Dk.Magufuli Kila Mahali.
????????????????????????????????????
Dk. John Pombe Magufuli Mgombea Urais kupitia CCM akisisitiza jambo wakati akihutubia mkutano wa kampeni uliofanyika Maili Moja mjini Kibaha jana.
????????????????????????????????????
Umati wa wananchi waliojitokeza katika mkutano wa Maili Moja Kibaha.
????????????????????????????????????
????????????????????????????????????
Mgombea Ubunge wa jimbo la Kibaha mjini Sylivester Koka akiwaomba kura wananchi wa jimbo lake katika mkutano wa kampeni uliofanyika Maili Moja mjini Kibaha.
????????????????????????????????????
Hawa nao walifanya yao
????????????????????????????????????
Mgombea ubunge wa jimbo la Chalinze Ndugu Ridhiwani Kikwete akiwaomba kura wananchi katika mkutano uliofanyika kata ya Bwilingu mjini Chalinze jana.
????????????????????????????????????
Mgombea ubunge wa jimbo la Kibaha vijijini Ndugu Hamod Jumaa akipiga Push Up huku Dk. John Pombe Magufuli akimuangalia katika mkutano uliofanyika mjini Mlandizi.
????????????????????????????????????
Dk. John Pombe Magufuli Mgombea Urais kupitia CCM akiondoka kwenye uwanja wa mkutano huo uliofanyika Bunju jimbo la Kawe jijini Dar es salaam.
????????????????????????????????????
Ulinzi ukiwa umeimarishwa vya kutosha katika mkutano huo.
Post a Comment