Friday, September 11, 2015

SERIKALI YAZINDUA UJENZI WA KITUO KIKUBWA CHA TIBA YA MOYO NCHINI

 Mkurugenzi wa Elimu ya juu kutoka Wizara ya Elimu na mafunzo ya Ufundi Stadi, Prof. Sylivia Temu akizungumza wakati wa uzinduzi mradi wa ujenzi wa kituo cha ubora wa sayansi ya magonjwa na mishipa ya moyo hapa nchini uliofanyika jijini Dar es Salaam jana. Kituo hicho kitakachokuwa na uwezo wa kutoa huduma za kitabibu na kitafiti kwenye magonjwa hayo kwa nchi zote za ukanda wa Afrika mashariki na kitakuwa chini ya usimamizi wa  Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili (MUHAS).
 Mkurugenzi wa Elimu ya juu kutoka Wizara ya Elimu na mafunzo ya Ufundi Stadi, Prof. Sylivia Temu (katikati waliokaa) akiwa kwenye picha ya pamoja na uongozi wa chuoChuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili (MUHAS), wawakilishi kutokakutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) pamoja na wadau mbalimbali wa sekta ya afya baada yauzinduzi mradi wa ujenzi wa kituo cha ubora wa sayansi ya magonjwa na mishipa ya moyo hapa nchini uliofanyika jijini Dar es Salaam jana. Kituo hicho kitakachokuwa na uwezo wa kutoa huduma za kitabibu na kitafiti kwenye magonjwa hayo kwa nchi zote za ukanda wa Afrika mashariki na kitakuwa chini ya usimamizi wa  (MUHAS).
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili (MUHAS), Prof Ephata Kaaya akizungumza wakati wa uzinduzi mradi wa ujenzi wa kituo cha ubora wa sayansi ya magonjwa na mishipa ya moyo hapa nchini uliofanyika jijini Dar es Salaam jana. Kituo hicho kitakachokuwa na uwezo wa kutoa huduma za kitabibu na kitafiti kwenye magonjwa hayo kwa nchi zote za ukanda wa Afrika mashariki na kitakuwa chini ya usimamizi wa  (MUHAS).

Muwakilishi kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika Bw. Demissie Dejene akizungumza wakati wa uzinduzi mradi wa ujenzi wa kituo cha ubora wa sayansi ya magonjwa na mishipa ya moyo hapa nchini uliofanyika jijini Dar es Salaam jana. Kituo hicho kitakachokuwa na uwezo wa kutoa huduma za kitabibu na kitafiti kwenye magonjwa hayo kwa nchi zote za ukanda wa Afrika mashariki na kitakuwa chini ya usimamizi wa  Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili (MUHAS)

Na Mwandishi wetu,
SERIKALI imezindua mradi wa ujenzi wa kituo cha ubora wa sayansi ya magonjwa na mishipa ya moyo hapa nchini kitakachokuwa na uwezo wa kutoa huduma za kitabibu na kitafiti kwenye magonjwa hayo kwa nchi zote za ukanda wa Afrika mashariki.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi huo uliofanyika jijini Dar es Salaam jana kwa niaba ya Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi stadi Bw. Shukuru Kawambwa, Mkurugenzi wa Elimu ya juu nchini, Prof. Sylivia Temu alisema mradi huo unaotekelezwa na serikali kwa ushirikiano na benki ya maendeleo ya Afrika  ni mojawapo ya miradi minne ya afya inayotekelezwa kwenye ukanda wa afrika mashariki ikilenga kutatua changamoto mbalimbali za kiafya.

No comments: