Wednesday, September 02, 2015

AIRTEL FURSA YAENDELA KUINUA VIJANA HAPA NCHINI

 Meneja wa Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (kulia),
akimkabidhi kijana Iddy Abdallah Chilumba, msaada wa mashine ya
kubangulia korosho vikiwemo meza, vifaa mbalimbali na pikipiki mpya,
kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’, katika hafla
iliyofanyika kwenye sehemu yake ya biashara iliyokarabatiwa na Airtel
katika Mtaa wa Relwe, Manispaa ya Mtwara jana. Wanaoshuhudia ni Meneja wa Airtel Mtwara, Bartholomew Masatu (wa pili kushoto), Meneja wa Huduma kwa Wateja wa Airtel, Happy John (wa tatu kushoto) na Afisa
Uhusiano na Matukio wa Airtel, Dangio Kaniki.
 Meneja wa Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (kulia),
akimkabidhi kijana Iddy Abdallah Chilumba, msaada wa vifaa mbalimbali
vya kubangulia korosho na pikipiki mpya, kupitia mpango wa Airtel
‘Fursa Tunakuwezesha’, katika hafla iliyofanyika kwenye sehemu yake ya
biashara iliyokarabatiwa na Airtel katika Mtaa wa Relwe, Manispaa ya
Mtwara jana. Wanaoshuhudia ni Meneja wa Airtel Mtwara, Bartholomew
Masatu (wa pili kushoto), Meneja wa Huduma kwa Wateja wa Airtel, Happy 
 John (wa tatu kushoto) na Afisa Uhusiano na Matukio wa Airtel, Dangio 
 
Kaniki.
 Meneja wa Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (kulia),
akimkabidhi kijana Iddy Abdallah Chilumba, msaada wa pikipiki mpya
vikiwemo vifaa mbalimbali vya kubangulia korosho, kupitia mpango wa
Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’, katika hafla iliyofanyika kwenye sehemu
yake ya biashara iliyokarabatiwa na Airtel katika Mtaa wa Relwe,
Manispaa ya Mtwara jana. Wanaoshuhudia ni Meneja wa Airtel Mtwara,
Bartholomew Masatu (wa pili kushoto), Meneja wa Huduma kwa Wateja wa
Airtel, Happy John (wa tatu kushoto) na Afisa Uhusiano na Matukio wa
Airtel, Dangio Kaniki.
 Meneja wa Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (kulia),
akimkabidhi kijana Iddy Abdallah Chilumba, kadi ya pikipiki mpya
iliyotolewa msaada kwake vikiwemo vifaa mbalimbali vya kubangulia
korosho, kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’, katika hafla
iliyofanyika kwenye sehemu yake ya biashara iliyokarabatiwa na Airtel
katika Mtaa wa Relwe, Manispaa ya Mtwara jana. Wanaoshuhudia ni Meneja wa Airtel Mtwara, Bartholomew Masatu (wa pili kushoto), Meneja wa Huduma kwa Wateja wa Airtel, Happy John (wa tatu kushoto) na Afisa
Uhusiano na Matukio wa Airtel, Dangio Kaniki.

Airtel Fursa Yaendela Kuinua Vijana hapa Nchini
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imemuwezesha mjasiriamali Idd
Chillumba vifaa vya kufanikisha shughuli zake za kufungasha Korosho
ikiwa ni pamoja na usafiri wa kuwezesha kusambaza bidhaa zake kwa
wateja wake kupitia mpango wake wa Airtel Fursa ambapo vitamuwezesha
kuinua maisha yake na familia yake.

Akikabidhi vifaa hivyo meneja wa huduma kwa jamii wa Airtel Bi Hawa
Bayumi amesema, vifaa hivyo vitamuwezesha Bw. Chillumba kuendeleza
biashara yake ya kufungasha Korosho na kusambaza kwa uharaka zaidi kwa 
 wateja wake.

Bi Bayumi amesema, mpango huo wa kuwawezesha wajasiriamali vifaa ni
sehemu ya mpango wa kampuni hiyo wa kuwawezesha vijana wenye malengo 
 mazuri na maisha yao, tabia nzuri, na wenye dhamira ya kujikomboa 
 
kimaisha na kuwa wafanyabiashara wakubwa hapo baadae.

“Sisi kama kampuni ya mawasiliano tumeona ni vizuri kushirikiana na
vijana ili kuhakikisha tunawawezesha na kukuza mitaji yao ya biashara
na kuweza kujiinua kiuchumi, kuweza kufikia ndoto zao na vile vile
kuongeza ajira kwa vijana hapa nchini” alisema meneja huyo.

“Vifaa hivi vitamuwezesha bw. Chillumba kuongeza biashara yake na
kupanua wigo wa kutoa huduma kwa wateja wake na  usafiri huu wa
pikipiki utampa nafuu ya kusafirishia bidhaa zake kutoka sehemu moja
kwenda nyingine.” aliongeza Bi Bayumi.

Akipokea msaada huo Bw. Chillumba ameshukuru kwa vifaa na usafiri huo
na kuahidi kuendeleza zaidi biashara hiyo ili kutimiza ndoto zake za
kuwa mfanyabiashara mkubwa.

“Sikuamini kama siku moja ningeweza kufikia malengo yangu katika
biashra hii. Mimi ni mtoto wa kwanza katika familia yetu.  Nilizaliwa
miaka ishirini na nne iliyopita. Baba yangu alifariki nikiwa na umri
wa mwaka mmoja. Mama yangu hakuwa na uwezo wa kunifikisha mbali
kielimu hivyo niliishia kidato cha nne.

 Ilinilazimu kuanza maisha
mapema kwa kuanzisha biashara ya kubangua korosho,  fedha ninayopata
japokuwa ni kidogo naitumia kujikimu mimi mwenyewe, kumsaidia mama
yangu na ndugu zangu. Kutokana na msaada huu kutoka Airtel, naahidi
kuongeza juhudi na kutumia vyema msaada huu ili kuhakikisha nakuza na
kuendeleza biashara yangu na kuinua vijana wenzangu hapo baadae”
alisema Chillumba.

Kampuni ya simu ya Airtel inazunguka nchi nzima kukutana na vijana kwa
lengo la kuwapa elimu ya ujasiriamali na asha kutoa uwezeshaji kwa

vijana ili waweze kukuza mitaji yao.

No comments: