Mgombea ubunge wa Arusha mjini kwa tiketi ya ACT WAZALENDO Ndugu Estomih Malla amefariki dunia usiku wa leo saa saba Oktoba 9, 2015 katika hospitali ya KCMC Moshi.
Ndugu Malla alipelekwa KCMC jana mchana kutokea Hospitali ya St. Thomas iliyopo Arusha mjini baada ya kulazwa hapo kwa siku mbili kwa sababu ya kupata tatizo la shinikizo la juu la damu.Hali hiyo ilimtokea siku ya tarehe 6/10/2015 mara baada ya kumalizika mkutano wa kampeni uliokuwa unafanyika Ngaramtoni,ambapo alilalamika kusikia kizunguzungu na baadae kukimbizwa hospital ya St Thomas ambapo madaktari wa pale walisema ndugu Malla anasumbuliwa na uchovu na hivyo anatakiwa kupumzika kwa muda mrefu.Kwa mujibu wa Afisa Habari wa Chama Cha ACT Wazalendo, Abdallah Khamis, ameithibitishia JamiiForums kutokea kwa kifo hicho na kwamba marehemu alifariki usiku huu wa Oktoba 9, 2015 saa Saba usiku.Amesema taarifa zaidi zitatolewa baadae baada ya uongozi wa chama hicho kufanya mawasiliano na viongozi waliopo mkoani Arusha.Sisi sote ni wa mola na hakika kwake sote tutarejea.
Friday, October 09, 2015
MGOMBEA UBUNGE KUPITIA ACT WAZALENDO ESTOMIH MALLA AFARIKI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
DKT. ABBASI AKAGUA MIRADI YA UTALII PORI LA AKIBA LA PANDE, ATOA MAAGIZO YA KUKAMILIKA KABLA YA AFCON 2027
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbasi, leo Julai 23, 2026, ametembelea Pori la Akiba la Pande jijini Dar es Salaa...
-
Hapa mmoja wa watoto hao akiwa na kijana mwenzake mwenye miaka 18, wote wako sawa lakini yeye hawezi kuzungumza kama watu wa kawaida. Mama S...
-
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu na timu ya Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa akiwa katika ...
-
Nadhani mtakumbuka kibwagizo maarufu katika TV ambacho kinaimbwa perupe pepero perupe pepero hawa ni vijana wa Sisi Tambala waliokuwapo kati...

No comments:
Post a Comment