Saturday, October 03, 2015

MAMA SALMA KIKWETE AZINDUA SHULE YA SEKONDARI J.K.NYERERE HUKO TARIME

1

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokewa rasmi na Mkuu wa Mkoa wa Mara Mheshimiwa Capt. Mstaafu Aseri Msangi mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Musoma kwa ziara ya siku mbili mkoani humo tarehe 2.10.2015. Aliyesimama kushoto ni Mwenyekiti wa Mkoa wa Mara.
2
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akishiriki kucheza ngoma ya utamaduni na wananchi wa Kijiji cha Nyamwaga kilichoko katika wilaya yaTarime kwa ajili ya kuzindua rasmi Shule ya Sekondari ya J. K. Nyerere iliyojengwa na Kampuni ya Acacia inayomiliki Mgodi wa North Mara Gold Mine tarehe 2.10.2015.
5
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akijumuika na viongozi wa Mkoa wa Mara na wanachi wa Kijiji cha Myamwaga kusherehekea uzinduzi rasmi wa Shule ya J.K. Nyerere iliyojengwa na North Mara Gold Mine.
4
Mke wan a Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA, Mama Salma Kikwete akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya ya Tarime Ndugu Glorius Luoga muda mfupi baada ya kuwasili kwenye Kijiji cha Nyamwaga kwa ajili ya uzinduzi wa Shule ya Sekondari J K Nyerere.
6
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akitoa hotua ya uzinduzi rasmi wa Shule ya Sekondari J.K.Nyerere katika Kijiji cha Myamwaga kilichoko Mkoani Mara.
8
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akishirikiana na viongozi wa Mkoa wa Mara na wale wa Wilaya ya Tarime na wahisani waliojenga Shule ya J.K. Nyerere kukata utepe ikiwa ni ishara ya uzinduzi rasmi wa Shule hiyo iliyoko katika Kijiji cha Nyamwaga.

No comments: