Thursday, October 08, 2015

LOWASSA AWATAKA WATANZANIA KUCHANGAMKIA FURSA ZA AJIRA ZITOLEWAZO NA AFRIKA MASHARIKI

WATANZANIA wametakiwa kujifunza kuchangamkia fursa za ajira zinazotolewa na Afrika Mashariki kama ilivyo kwa nchi nyingine.
Kauli hiyo ilitolewa jana na mgombea wa Urais kupitia Chadema, Edward Lowassa alipokuwa kwenye kampeni zake zilizofanyika katika uwanja wa Shule ya Msingi Namanga.
Lowassa alisema iwapo atachaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, atahakikisha kuwa watanzania wanachangamkia fursa za Afrika Mashariki kama ilivyo kwa Kenya.
“Napenda mahusiano ya Afrika Mashariki yawe ya kweli na siyo upande mmoja unafaidi na mwingine haufaidi,”alisema na kuongeza kuwa:
“Watanzania wakiwa wanapita kwenye mpaka wa Namanga wasisumbuliwe wapite bila shida.”
Sehemu ya wananchi wa eneo la Kisongo, Jijini Arusha wakiwa wamefunga barabara kuzuia msafara wa Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, ili waweze kumsalimia na kumsikiliza, wakati alipokuwa njiani kuelekea eneo la Ngaramtoni mpaka Namanga, kwenye Mkutano wa Kampeni, jana Oktoba 7, 2015.
PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI, ARUSHA.
Hivi ndivyo hali ilivyokuwa kwa vijana wa eneo la Kisongo, walipokuwa wakimsindikiza mpendwa wao.
Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, akiwasili kwenye Uwanja wa Shule ya Sekondari Mringa, Jimbo la Arumeru Magharibi, Jijini Arusha jana Oktoba 7, 2015, kulikofanyika Mkutano wa Kampeni zake.
Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, akiwapungia wananchi wa Jimbo la Arumeru Magharibi waliohudhulia Mkutano wa Kampeni zake, uliofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Sekondari Mringa, Jimbo la Arumeru Magharibi, Jijini Arusha jana Oktoba 7, 2015.
Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, akiwahutubia wananchi wa Jimbo la Arumeru Magharibi katika Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Sekondari Mringa, Jimbo la Arumeru Magharibi, Jijini Arusha jana Oktoba 7, 2015.
Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, akiwapungia wananchi wa Jimbo la Longido waliohudhulia Mkutano wa Kampeni zake, uliofanyika kwenye Uwanja wa Namanga, Jijini Arusha jana Oktoba 7, 2015.

No comments: