Friday, November 06, 2015

MULTICHOICE TANZANIA WAMTANGAZA RASMI DIAMOND PLATNUMZ KUWA ‘OFFICIAL DSTV BRAND AMBASSADOR’

DSC_0168Mwanamuiki nyota nchini Tanzania, Nassib Abdul ama Diamond Platnumz akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani). (Picha na Andrew Chale, Modewjiblog).
KAMPUNI ya MultiChoice Tanzania mapema jana imezindua ofa kabambe za msimu wa siku kuu huku ikimtambulisha rasmi Mwanamuziki Diamond Platnumz kuwa balozi maalum wa bidhaa za kampuni hiyo ikiwemo kifurushi cha DSTV BOMBA chenye chaneli zaidi ya 65 ikiwemo huduma ya vituo kadhaa vya televisheni za hapa nchini.
Akimtambulusha rasmi Meneja Masoko wa kampuni hiyo, Furaha Samalu, amemtambulisha Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kuwa balozi wa king’amuzi hicho na kutaja gharama zake kuwa ni shilingi 23,500/= kwa malipo ya mwezi na king’amuzi chenyewe kinapatikana kwa shilingi 79,000/= na kuwataka wananchi kuchangamkia huduma hiyo muhimu katika msimu huu wa ofa za sikukuu.
Meneja masoko huyo ameongeza kuwa, kifurushi hicho kimesambaa nchini mbalimbali barani Afrika hivyo wasanii wa filamu, muziki na wengineo ambao watang’aa kwenye vipindi hivyo watakuwa wakionekana pande mbalimbali barani Afrika na hivyo kuwapatia umaarufu na kuwaongezea soko la kazi zao.
DSC_0151Mwanamuziki Diamond Platinumz akisoma kipeperushi chenye maelezo juu ya ofa mbalimbali za DStv wakati wa utambulisho wa ofa za sikukuu pamoja na kutangazwa kwa balozi huyo wa bidhaa za DSTV. Katikati Afisa Masoko wa Multichoice Tanzania, Furaha Samalu na kushoto ni Meneja Mwendeshaji wa Multichoice Tanzania, Ronald Baraka Shelukindo.
DSC_0233Meneja Masoko wa Multichoice Tanzania, Furaha Samalu akifafanua jambo katika mkutano huo na kushoto ni Meneja Mwendeshaji wa Multichoice Tanzania, Ronald Baraka Shelukindo na upande wa kulia ni msanii Diamond Platnumz balozi wa bidhaa za DSTV.
DSC_0159Meneja mauzo wa DSTV, Bw. Salum Salum akifafanua jambo juu ya ofa hiyo mpya na mahaala wanapopatikana nchini kwa mawakala wote ambapo amewaomba watanzania kuchangamkia ofa ya kuunganishwa haraka huduma bora zaidi za chaneli za kisasa kupitia DSTV.
DSC_0174Baadhi ya wanahabari wakifuatilia mkutano huo wa DSTV..
DSC_0176Mwandishi wa gazeti la Raia Tanzania akiuliza swali juu ya bidhaa za DSTV..
DSC_0171Mpiga picha wa Magazeti ya Habari leo, Fadhili Akida akiuliza swali katika mkutano huo wa DSTV..
DSC_0185Ilifika wakati wa zawadi.. Diamond akisoma jina la mwandishi wa habari aliyeshinda zawadi hiyo..
DSC_0190Diamond Platnumz akimkabidhi mwandishi wa habari, Sangu Joseph king’amuzi alichojishindia katika droo iliyochezeshwa wakati wa mkutano huo.
DSC_0196Diamond akikabidhi zawadi ya King’amuzi cha DSTV kwa mwandishi wa habari Rajab Musa baada ya kushinda..
DSC_0204Diamond akikabidhi zawadi ya king’amuzi kwa mwandishi wa habari, Joseph Mchekadone baada ya kushinda..
DSC_0205Diamond Platnumz akimkabidhi king’amuzi mwanahabari wa ITV, Ester Sangai baada ya kuibuka mshindi..
DSC_0165Meneja mauzo wa DSTV, Bw. Salum akisisitiza juu ya ofa hiyo ambapo ameeleza kuwa wateja watapa kujionea chaneli mbalimbali zenye mvuto na picha za kuvutia huku bidhaa zake zikiwa ni tofauti kabisa na zingine.

No comments: