Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika Bibi Sophia Kaduma ameiagiza Bodi ya Sukari Tanzania, kushughulikia mara moja madai ya wakulima wadogo wa miwa (outgrowers) katika Kiwanda cha Sukari cha Kilombero kilichopo Mkoani Morogoro yaliotokana na miwa yao kutonunuliwa na kiwanda.
Katika agizo hilo, Katibu Mkuu Bibi Sophia Kaduma ameiagiza Bodi ya Sukari Tanzania kukuta na Uongozi wa Kiwanda cha Sukari cha Kilombero na ule wa wakulima wadogo wa miwa ili kupata ufumbuzi wa kudumu kuhusu soko la miwa wanayozalisha.
Aidha, Katibu Mkuu ametoa muda wa siku saba kwa Bodi ya Sukari Tanzania iwe imetekeleza na kutoa taarifa ya utekelezaji wa agizo hilo.
Agizo hilo limekuja kufuatia Serikali kupata taarifa kuwa Uongozi wa Kiwanda hicho umeshindwa kununua miwa ya wakulima hao licha ya makubaliano yao ya awali ya kuzalisha miwa na kukiuzia kiwanda kwa ajili ya kuzalisha sukari. Wakulima wamedai kuwa miwa hiyo, inakadiriwa kuwa na thamani ya zaidi ya shilingi milioni 16.
Bodi ya Sukari Tanzania imeanzishwa kwa mujibu wa Sheria ya Sukari Na. 26 ya mwaka 2001 kama ilivyorekebishwa mwaka 2009 na Sheria ya Marekebisho ya Sheria za Mazao Na. 20 ya mwaka 2009 (Crop Laws (Miscellenous Amendments) Act).

Bodi ya Sukari Tanzania inajukumu pamoja na mambo mengine, kusimamia na kuratibu kilimo cha miwa na biashara ya sukari nchini, kusajili wakulima, wazalishaji wa sukari na wafanyabiashara wa sukari.
Aidha, Bodi ya Sukari ina dhamana ya kuhakikisha uwepo wa ushindani wa haki kwenye soko la miwa na biashara ya sukari nchini.
Aidha, Bodi ya Sukari ina dhamana ya kuhakikisha uwepo wa ushindani wa haki kwenye soko la miwa na biashara ya sukari nchini.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali
Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika
Kilimo Complex,
1 Mtaa wa Kilimo 15471
DAR ES SALAAM
Comments