Friday, November 06, 2015

TNRF WAMTAKA MAGUFULI ADHIBITI UPOTEVU WA MALIASILI NCHINI

 Mwenyekiti wa Jumuiko la Maliasili nchini (TNRF) ,Dr.Suma Kaare akizungumza katika mkutano wa 7 wa jumuiko hilo uliofanyika jijini Arusha na kuhudhuriwa na mashirika binafsi pamoja na wawakilishi kutoka wizara ya maliasili.Picha na Gadiola Emmanuel
  Mkurugenzi wa Shirika la Haki kazi Catalyst Alais Moridant akifafanua jambo  katika mkutano wa 7 wa jumuiko hilo uliofanyika jijini
Arusha na kuhudhuriwa na mashirika binafsi pamoja na wawakilishi kutoka
wizara ya maliasili.Picha na Gadiola Emmanuel
  Mkurugenzi wa Shirika la AWF ,John Salehe
akifafanua jambo  katika mkutano wa 7 wa jumuiko hilo uliofanyika jijini
Arusha na kuhudhuriwa na mashirika binafsi pamoja na wawakilishi kutoka
wizara ya maliasili.Picha na Gadiola Emmanuel
  Washiriki wa  mkutano wa 7 wa jumuiko la maliasili  uliofanyika jijini

  Viongozi mbalimbali wa jumuiko la maliasili wakiwa katika mkutano wa 7 wa jumuiko hilo uliofanyika jijini
Arusha na kuhudhuriwa na mashirika binafsi pamoja na wawakilishi kutoka
wizara ya maliasili.Picha na Gadiola Emmanuel
 Washiriki wa  mkutano wa 7 wa jumuiko la maliasili  uliofanyika jijini
Arusha wakiwa katika picha ya pamoja, ,mkutano huo ulihudhuriwa na mashirika binafsi pamoja na wawakilishi kutoka
wizara ya maliasili.Picha na Gadiola Emmanuel
Washiriki wa  mkutano wa 7 wa jumuiko la maliasili  uliofanyika jijini
Arusha na kuhudhuriwa na mashirika binafsi pamoja na wawakilishi kutoka
wizara ya maliasili.Picha na Gadiola Emmanuel 
Washiriki wa  mkutano wa 7 wa jumuiko la maliasili  uliofanyika jijini
Arusha na kuhudhuriwa na mashirika binafsi pamoja na wawakilishi kutoka
wizara ya maliasili.Picha na Gadiola Emmanuel 
Mwakilishi wa Shirika la WWF ,Sware Semesi  akizungumza katika  mkutano wa 7 wa jumuiko la maliasili  uliofanyika jijini
Arusha na kuhudhuriwa na mashirika binafsi pamoja na wawakilishi kutoka
wizara ya maliasili.Picha na Gadiola Emmanuel 
 Washiriki wa  mkutano wa 7 wa jumuiko la maliasili  uliofanyika jijini
Arusha na kuhudhuriwa na mashirika binafsi pamoja na wawakilishi kutoka
wizara ya maliasili.Picha na Gadiola Emmanuel
Wasemaji Wakuu wa   mkutano wa 7 wa jumuiko la maliasili  uliofanyika jijini
Arusha na kuhudhuriwa na mashirika binafsi pamoja na wawakilishi kutoka
wizara ya maliasili.Picha na Gadiola Emmanuel 
Na Ferdinand Shayo wa Wazalendo 25 Blog ,Arusha.
Mwenyekiti
wa Jumuiko la Maliasili nchini Dr.Suma Kaare amemtaka Raisi John Pombe Magufuli
adhibiti upotevu wa mali asili za wanyama pori na misitu uliokithiri katika
maeneo mengi nchini ili kunusuru uhai wa maliasili.
Suma Kaare
amesema  hayo katika mkutano wa 7 wa
jumuiko la maliasili  unaoendelea jijini
Arusha,Kaare amesema kuwa jukwaa hilo litashirikiana na Rais huyo katika  kuhakikisha kuwa maliasili zinalindwa na
kuwanufaisha Watanzania kwa kiwango stahiki.
“Tunajua
Rais wetu mpya ana kazi  kubwa  ya kulinda maliasili za nchi hii kama ilivyo
kauli mbiu yake ya “kazi tu” tunaamini atazuia upotevu mkubwa wa rasilimali
unaofanywa na watendaji wasio waaminifu” Alisema Kaare
Mratibu wa
Masuala ya misitu katika shirika la uhifadhi wa maliasili na Mazingira (wwf)
,Isaac Malungu amesema kuwa asilimia 90% ya nishati inayotumika nchini
inatokana na kuni pamoja na mkaa hali ambayo inaathiri misitu na kutishia uhai
wa maliasili nchini hivyo ameitaka serikali ihimize matumizi ya nishati mbadala
ili kunusuru mazingira yanaoharibiwa kila kukicha.
Malungu alisema
kuwa kilimo cha kuhama hama pamoja na ukataji miti ovyo umekua ukisababisha
uharibifu wa mazingira na hata kupelekea hecta laki 4 za misitu kupotea kila
mwaka kutokana na shughuli hizo.
Mkurugenzi
wa  Shirika la AWF,John Salehe Alisema
kuwa mabadiliko ya tabia ya nchi yamesababisha hali ya ukame inayowaathiri
wanyama pamoja na mimea hivyo kuathiri uhifadhi kwa ujumla .
Salehe
alisema kuwa juhudi zaidi zinapaswa kuchukuliwa ikiwemo upandaji wa miti pamoja
na kutunza misitu ili kurejesha uoto wa asili uliopotea.

No comments: