Saturday, November 07, 2015

Serikali yasitisha matumizi ya Picha Rasmi ya Rais Magufuli


Serikali inapenda kuzitaarifu ofisi za umma  na  wananchi  kwa ujumla  kwamba  imesitisha    matumizi  ya  picha ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  wa Serikali ya Awamu ya Tano, Mhe.Dkt. John  Pombe Josep Magufuli mpaka hapo itakapotangazwa tena.

Awali   majira ya saa 6: 00 mchana leo Novemba 6, mwaka huu Serikali ilitangaza kuhusu kuanza rasmi kwa matumizi ya picha ya Rais.


Aidha,   Serikali  imesema kwamba  itazitangazia  ofisi hizo na umma wa Watanzania  kuhusu kuanza tena  kwa  matumizi ya picha  hiyo hapo baadae.

Imetolewa na
IDARA YA HABARI.
Novemba 6,mwaka 2015

No comments: