Friday, November 06, 2015

SIKU YA KWANZA YA DK. MAGUFULI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akisalimiana na wanausalama alipowasili Ikulu mara baada ya Kuapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe
Magufuli (Katikati) Akiongozana na Mkewe Mama Janet Magufuli
walipowasili Ikulu mara baada ya Kuapishwa kwenye sherehe zilizofanyika
katika uwanja wa Uhuru jana Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe
Magufuli akisalimiana na wafanyakazi wa Ikulu mara baada ya kuapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania


Ngoma kama ishara ya kumkaribisha Ikulu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli mara baada ya kuapishwa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akiwaongoza baadhi ya marais wa Afrika Kuimba wimbo wa Taifa, Kushoto kwake ni Rais wa Tanzania aliyemaliza muda wake Dk. Jakaya Mrisho Kikwete
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janet Magufuli na Mke wa Rais aliyemaliza muda wake Mama Salma Kikwete wakiwa katika hafla iliyofanyika mapema jana Ikulu Dar es Salaam
Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Ally Mohamed Shein akimueleza jambo Rais wa Kenya Uhuru Kenyata wakati wa hafla iliyofanyika jana Ikulu Jijini Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akiteta jambo na Rais wa Uganda Yoweri Museveni
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya Pamoja na baadhi ya viongozi wa nchi za afrika na wawakilishi wa mataifa mengine duniani katika hafla iliyofanyika jana Ikulu Jijini Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma, Kulia ni Rais aliyemaliza muda wake Dk. Jakaya Kikwete na Kulia ni Mke wa Rais Mteule Mama Janet Magufuli
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli katika picha ya pamoja na Rais wa Kenya Uhuru Kenyata, Raila Odinga na wake zao
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akiagana na Rais wa Kenya Uhuru Kenyata jana Ikilu Jijini Dar es Salaam
Raila Odinga akimkumbatia Rais wa Kenya Uhuru Kenyata katika hafla iliyofanyika jana Ikulu Jijini Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mke wa Raila Odinga, na Mama Janet Magufuli akisalimiana na Raila Odinga wakati wa Hafla iliyofanyika jana Ikulu Jijini Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akiwaeleza Jambo Rais wa Kenya Uhuru Kenyata na Rais aliyemaliza Muda wake Dk. Jakaya Mrisho Kikwete jana Ikulu Jijini Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Rais wa awamu ya Pili Alhaj Ally Hassan Mwinyi na Rais wa awamu ya nne Dk. Jakaya Mrisho Kikwete Ikulu jana Jijini Dar es Salaam
(Picha na Hassan Silayo-MAELEZO)
Post a Comment