NAIBU KATIBU MKUU WA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI ATEMBELEA MAKAO MAKUU YA JESHI LA POLISI NA KUWAPONGEZA KWA KUSIMAMIA UCHAGUZI MKUU KWA AMANI NA UTULIVU
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, John Mngodo, akizungumza na
Maafisa wa Jeshi la Polisi, wakati wa mkutano wa Kujitambulisha na kufahamiana
na Watendaji wakuu na Maafisa wa Jeshi la Polisi uliofanyika Makao Makuu ya
Jeshi hilo, jijini Dar es Salaam leo. Katika hotuba yake, Mngodo alilipongeza
jeshi hilo kwa kusimamia Uchaguzi Mkuu kwa amani na utulivu. Kulia kwa Katibu
Mkuu ni Inspekta Jenerali wa Jeshi hilo (IGP), Ernest Mangu.
Inspekta
Jenerali wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Ernest Mangu (kushoto) akiwaongoza
watendaji wakuu na maafisa wa jeshi hilo kuimba wimbo wa maadili wa jeshi hilo
wakati wa ziara ya Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, John
Mngodo (wapili kushoto). Ziara hiyo iliyofanyika Makao Makuu ya jeshi hilo
jijini Dar es Salaam leo, ilikuwa na lengo la kujitambulisha na kufahamiana na
watendaji hao. Watatu kushoto meza kuu ni Naibu IGP, Abdulharam Kaniki, wapili
kulia ni Kamishna wa Lojistiki na Fedha wa Jeshi la Polisi Clodwig Mtweve, na
kulia ni Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Suleiman
Kova.
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, John Mngodo, akizungumza na Watendaji
wakuu na Maafisa wa Jeshi la Polisi nchini wakati alipofanya ziara Makao Makuu
ya Jeshi hilo jijini Dar es Salaam leo kwa lengo la kujitambulisha na
kufahamiana na watendaji hao. Kushoto meza kuu ni Inspekta Jenerali wa Jeshi la
Polisi nchini (IGP), Ernest Mangu, Watatu kushoto meza kuu ni Naibu IGP,
Abdulharam Kaniki, wapili kulia ni Kamishna wa Lojistiki na Fedha wa jeshi
hilo, Clodwig Mtweve, na kulia ni Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es
Salaam, Kamishna Suleiman Kova.
Inspekta
Jenerali wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Ernest Mangu (kushoto) akitoa taarifa
ya Jeshi hilo wakati wa Ziara ya Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani
ya Nchi, John Mngodo, alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi hilo jijini Dar es
Salaam kwa lengo la kujitambulisha na
kufahamiana na watendaji wa jeshi hilo.
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, John Mngodo (kulia), akiagana
na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Suleiman Kova baada
ya kumaliza ziara yake katika Makao Makuu ya jeshi hilo jijini Dar es Salaam. Katikati
ni Kamishna wa Lojistiki na Fedha wa jeshi hilo, Clodwig Mtweve, wapili kushoto
ni Kamishna wa Polisi Jamii nchini, Musa Ali Musa, akifuatiwa na Mkurugenzi wa
Upelelezi wa Makosa ya Jinai, Diwani Athumani.
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, John Mngodo ( watano kulia),
Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Ernest Mangu (watano
kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na Watendaji wakuu na Maafisa wa jeshi hilo
muda mfupi baada ya kumaliza ziara ya kutembelea Makao Makuu ya Jeshi hilo
jijini Dar es Salaam leo. Picha
zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Comments