Thursday, November 26, 2015

BARAZA LA UJENZI ENDELEVU NA MAZINGIRA TANZANIA LATANGAZA AZMA YAKE UJENZI ENDELEVU

Viongozi wa Baraza la Ujenzi Endelevu na Utunzaji wa Mazingira Tanzania, Afisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Baraza hilo, Ipyana Moses na Makamu wa Rais wa Baraza hilo, Farizan d’Avezac de Moran wakijadiliana jambo na Mkurugenzi wa Ubunifu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Issack Peter (katikati) nje ya makao makuu ya Shirika la Nyumba la Taifa, NHC Place jijini Dar es Salaam leo.
 Viongozi wa Baraza la Ujenzi Endelevu na Utunzaji wa Mazingira TanzaniaAfisa Mtendaji Mkuu wa Baraza hilo, Ipyana Moses na Makamu wa Rais wa Baraza hilo, Farizan d’Avezac de Moran wakijadiliana jambo na Mkurugenzi wa Ubunifu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Issack Peter (katikati) nje ya makao makuu ya Shirika la Nyumba la Taifa, NHC Place jijini Dar es Salaam leo.
 Viongozi wa Baraza la Ujenzi Endelevu na Utunzaji wa Mazingira TanzaniaAfisa Mtendaji Mkuu wa Baraza la Ujenzi Endelevu na Utunzaji wa Mazingira Tanzania Ipyana Moses na Makamu wa Rais wa Baraza hilo, Farizan d’Avezac de Moran wakijadiliana jambo na Mkurugenzi wa Ubunifu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Issack Peter (katikati) nje ya makao makuu ya Shirika la Nyumba la Taifa, NHC Place jijini Dar es Salaam leo.
 Afisa Mtendaji Mkuu wa Baraza la Ujenzi Endelevu na Utunzaji wa Mazingira Tanzania, Ipyana Moses akizungumzia kongamano azma yao hiyo jijijni Dar leo.
 Afisa Mtendaji Mkuu wa Baraza la Ujenzi Endelevu na Utunzaji wa Mazingira Tanzania, Ipyana Moses akizungumzia kongamano azma yao hiyo jijijni Dar leo.
Alama ya ubora ya Ujenzi Endelevu na Utunzaji wa Mazingira ambayo Shirika la Nyumba la Taifa limetunukiwa na Mamlaka ya Ujenzi Endelevu ya Singapore BCA ni alama ya ubora wa kimataifa ambayo ni mpya kabisa kuanzishwa duniani.
Baraza la Ujenzi Endelevu na Utunzaji wa Mazingira Tanzania (Green Building Council of Tanzania) limetangaza azma yake ya kuhakikisha linafanyia kazi mita za mraba 330,000 za majengo kwa kipindi cha miaka mitano ijayo kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kutoka sekta ya fedha ili kuzishawishi zitoe mikopo kwa wadau waweze kujenga majengo yanayozingatia utunzaji wa mazingira na matumizi bora ya nishati.
Baraza hilo limetangaza azma hiyo likisema kuwa hiyo ndiyo itakayokuwa ajenda kuu ya Tanzania kwenye kongamano la 21 la nchi wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi. Mkataba huo ulisainiwa kwenye kongamano la dunia la Rio mwaka 1992 na kuridhiwa na nchi 195 mwaka 1994. Pia kongamano hilo ni mkutano wa 11 wa nchi wanachama wa mkataba wa Kyoto kuhusu kupunguza utoaji wa gesi chafuzi.
Akizungumza ajenda hizo, Afisa Mtendaji Mkuu wa Baraza hilo, Ipyana Moses alisema kuwa wao kama Green Building wameweka azma kufanyia kazi mita za mraba 330,000 majengo yanayojengwa ili yawe enedelevu kwa kipindi cha miaka mitano ijayo kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kutoka sekta ya fedha ili kutoa mikopo kujenga majengo yanayotumia nishati kwa kiasi kidogo.
Shirika la Nyumba la Taifa ni mmoja wa waasisi wa Baraza hil. Baraza lina wadau wengi wakiwamo Wasanifu Majenzi , Wakadiriaji majengo, wahandisi watengenezaji vifaa na watumiaji wa vifaa. Baraza hilo lilizinduliwa mapema mwezi Februari mwaka huu.
Nani atahudhuria COP21 ?
Watu wapatao 45,000 wanatarajiwa kuhudhuria mkutano huo utakaoanza tarehe 30, Novemba hadi Disemba tarehe 11 mwaka huu wa 2015. Na mkutano utafanyika eneo liitwalo Le Bourget, kwenye viunga vya mji mkuu wa Ufaransa, Paris.
Ni matokeo gani yanayotarajiwa?
Kuna mambo makubwa matatu:
Mosi; Ni makubaliano ambayo yatakuwa na nguvu kisheria kuhusu mabadiliko ya tabianchi.
Pili; Ni mwafaka kuhusu michango ya mambo yanayotarijiwa kutekelezwa kitaifa (INDCs). Kila nchi mwanachama inatarajiwa kutangaza mchango wake na kuutekeleza.
Na tatu ni mpango wa ufadhili ili kusaidia nchi zinazoendelea kutekeleza makubaliano hayo.
Nchi ngapi zimeshatangaza michango yao ?
Kufikia tarehe 31, Oktoba mwaka huu, tayari nchi 155 zimeshatangaza michango yao ya kitaifa, ikiwa ni sawa na asilimia 90 ya uzalishaji wote wa gesi chafuzi duniani. Nchi zote za Afrika Mashariki zimeshatangaza michango yao.
Na kuna tovuti inayorodhesha nchi zote na michango yao.

Post a Comment