Waziri Mkuu mpya Mh. Kassim Majaliwa.
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, muda mfupi uliopita limepitisha jina la Mbunge wa Jimbo la Rwangwa, Mh. Kassim Majaliwa kuwa Waziri Mkuu wa kwanza wa Serikali ya awamu ya tano baada ya jina lake kupelekwa Bungeni na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.
Awali Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli alimteua Mh. Kassim Majaliwa Mbunge wa Ruangwa mkoa wa Lindi na Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu Tamisemi anayeshughulia elimu kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Akitangaza jina hilo Spika wa Bunge Mh. Job Ndugai amewaeleza wabunge kuwa kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inampa rais kuteua jina la Waziri Mkuu na kuliwasilisha bungeni kwa ajili ya kuthibitishwa na wabunge
Hivyo bunge litamthibitisha rasmi na kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Fullshangwe na kikosi chake chote kimatakia Mh. Waziri Mkuu Mteule Kassim Majaliwa afya njema na mafanikio katika majukumu yake mapya.
No comments:
Post a Comment