Monday, November 23, 2015

CCM YASHINDA UBUNGE MAJIMBO YA ULANGA NA LUSHOTO.


Aliyekuwa mgombea wa kiti cha ubunge katika jimbo la Ulanga kupitia CCM, Mlingwa Goodluck ameshinda kiti hicho baada ya kupata kura 25,902 sawa na asilimia 69.7 ya kura halali zilizopigwa.
Msimamizi wa uchaguzi jimbo hilo Bi Isabela Chilumba amemtanganza Mlingwa Goodluck wa CCM kuwa mshindi wa ubunge na kuwazidi Michael Ikongoli aliyepata wa CHADEMA aliyepata kura 10,592 sawa na asilimia 28.5, na Isaya Mputa wa ACT Wazalendo aliyepata kura 626 sawa na asilimia 1.7.
Chilumba amesema kuwa idadi ndigo ya watu imejitokeza kupiga kura, ambapo watu 37,120 pekee ndiyo waliopiga kura kati ya watu 76,715 waliojiandikisha.
Aidha katika jimbo la Lushoto, Msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo Juma Shauri, amemtangaza Shaaban Shekilindi wa CCM kuwa mshindi wa kiti hicho baada ya kupata kura 19,775 sawa na asilimia 79.1.
Shekilindi amewapiku Juma Dickson wa CHADEMA aliyepata kura 4,402 sawa na asilimia 17.6, Maajabu Kusaga wa ACT aliyepata kura 375 sawa na asilimia 1,5 na Kahoneka Adam wa CUF aliyepata kura 350 sawa na asilimia 1.4.
Matokeo haya yanaifanya CCM kufikisha majimbo matatu kati ya majimbo 8 ambayo uchaguzi wa ubunge haukufanyika likiwemo jimbo la Lilindi wilayani Masasi mkoani Mtwara, kufikisha jumla ya majimbo 191 bungeni.
Majimbo ambako uchaguzi bado haujafanyika ni pamoja na Arusha Mjini, Handeni Mjini, Ludewa Masasi Mjini na Kijito Upele Zanzibar.
Post a Comment