Thursday, November 26, 2015

AIRTEL TANZANIA YAPIGA ‘TAFU’ TASWA SC

indexMeneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando akimkabidhi vifaa vya michezo Mwenyekiti wa timu ya waandishi wa habari za michezo nchini (Taswa SC) Majuto Omary kwa ajili ya kutumika katika mechi zao.
……………………………………………………………………………………………
Kampuni ya Airtel Tanzania imeiipiga ‘tafu’ timu ya soka na netiboli ya waandishi wa habari za michezo nchini, Taswa SC kwa kuwapatia vifaa vya michezo.
Akizungumza katika makabidhiano hayo jana,  Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando alisema kuwa kampuni yao inatambua mchango wa waandishi wa habari za michezo nchini katika kuendeleza michezo na kuamua kutoa vifaa vya michezo ambazo ni seti mbili za jezi na mipira.
Mmbando alisema kuwa mbali ya kuwa wadau wakubwa wa michezo, msaada huo ni moja ya muendelezo wao katika shughuli za kijamii.
“Airtel Tanzania ni wadau wakubwa wa michezo na burudani, tumeshiriki katika shughuli mbali mbali ikiwa kuendesha michezo ya Airtel Rising Stars, tumeamua kuunga mkono juhudi za timu ya waandishi wa habari za
michezo kuwakutanisha wana-habari na kushiriki katika mazoezi na mechi kwa ajili ya kuhamasisha vipaji na afya zao,” alisema Mmbando.
Mwenyekiti wa Taswa SC, Majuto Omary aliishukuru Airtel Tanzania kwa msaada huo ambao umetokana na maombi yao kwa kampuni hiyo.
Majuto alisema kuwa Taswa SC kwa kujua wadau wake, waliamua kuomba msaada wa vifaa hivyo na Airtel Tanzania kuwajali na kuchukua juhudi za haraka kutoa mchango wao.
“Tumeomba kwa  kampuni nyingi, bado  hatujapata majibu ya kukubaliwa au la, Airtel Tanzania imeonyesha mfano kwa kutusaidia kwa haraka sana, ni faraja kwetu, tunawaomba wengine waige mfano wao,” alisema Majuto.
Alisema kuwa Taswa SC bado inakabiliwa na changamoto ya vifaa vingine kama viatu kwa timu zake za soka na netiboli na kuwaomba wadau wafikirie kuwasaidia. “ Tupo tayari kupokea vifaa vingine, timu
inatakiwa kuwa na vifaa vya kutosha, jezi za aina mbalimbali, mipira ya mazoezi na mechi, hivyo kama kuna wadau wanataka kutusaidia, wasisite kufanya hivyo,” alisisitiza Majuto.
Post a Comment