Mbunge wa Jimbo la Ilala Mussa Zungu (CCM) (mwenye kofia) akimkabidhi nahodha wa timu ya Ferry Beach Boys, Selemani Ally ‘Kaseja’ nyaraka za Pikipiki Dar es Salaam leo ambayo ilikuwa ni moja ya ahadi yake kwa kikosi hicho wakati wa kampeni.(PICHA NA KHAMISI MUSSA)
Mbunge wa Jimbo la Ilala Mussa Zungu (CCM) (mwenye kofia) akimkabidhi nahodha wa timu ya Ferry Beach Boys, Selemani Ally ‘Kaseja’ kibao cha namba za Pikipiki Dar es Salaam leo.
Zungu amesema ilikuwa ni moja ya ahadi yake kwa kikosi hicho wakati wa kampeni alipofika kituoni hapo wakati alipopita kumuombea kura aliyekuwa mgombea Urais Dk John Pombe Mgufuli kupitia Chama cha Mapinduzi CCM ili iwasaidie kuongeza kipato.
Mbunge huyo aliendelea kusema ataendelea kusaidia maswala ya michezo ili kuinua sekta hiyo kwa kusaidia vifaa vya michezo Zungu ameongeza na kusema ” Leo nakusaidieni Pikipiki iwe mali ya timu si mali ya mtu,ya wafanyabiashara wenyewe, na niliweka ahadi ya kuwawekea mahema kwenye maeneo mnayouzia samaki, Nitatekeleza hilo kabla ya mwezi wa kumi na mbili ili mfanye biashara kwa uhuru.
Comments