Tuesday, November 24, 2015

MAFUNDI WAZISHUGULIKIA MASHINE ZA MRI NA CT-SCAN MUHIMBILI.


MAFUNDI kutoka kampuni ya Philips wanaendelea na matengenezo ya mashine za MRI na CT-SCAN katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili zilizopata hitilafu za kiufundi hivi karibuni.

Akizungumza ofisini kwake leo hii Mkuu wa Idara ya Uhusiano Hospitali ya Taifa Muhimbili Bw. Aminiel Buberwa Aligaesha amesema mafundi wapo katika eneo la kazi wakitengeneza hizo mashine ili ziweze kurudi katika hali yake ya kawaida.

“Tumepewa siku tatu kukamilisha ukarabati wa hizi mashine hivyo wananchi wawe na subira kwani mashine zikiwa tayari kwa matumizi tutatoa  taarifa” alisema Aligaesha.

Ameongeza kuwa wananchi wawape muda waweze kuzitengeneza mashine hizo ili ziweze kutengemaa kwa ajili ya kutoa huduma za MRI na CT-SCAN hospitalini hapo.

Mashine za MRI na CT-SCAN zilianza kufanya kazi  mara baada ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Joseph Magufuli kutembelea hospitali hiyo hivi karibuni na kuagiza kutengenezwa kwa mashine hizo na baadae kufanya kazi kwa muda wa siku kadhaa na kuharibika tena kutoka na hitilafu za kiufundi.

Wakati alipotembelea Hospital ya Taifa ya Muhimbili jana Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue aliagiza mashine hizo kutengenezwa,  ndani ya siku tatu  ziwe zimekamilika kwa ajili ya kutoa huduma kwa wananchi.

Hospitali ya Taifa ya Muhimbili imekuwa ni kimbilio la wananchi wengi kupata huduma za afya hivyo serikali inapamabana kwa kila hali kuhakikisha huduma za MRI na CT-SCAN zinarudi katika hali yake ya kawaida hospitalini hapo.

No comments:

RUZUKU YA SH.MILIONI 250 YATOLEWA KWA WABUNIFU WA MATUMIZI BORA YA NISHATI

📌 Kamishna wa Umeme asema Serikali itaendelea kuwawezesha vijana wabunifu katika teknolojia ya matumizi bora ya nishati 📌 Wabunifu wa kike...